Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 22, 2013

STAR TIMES KUBURUDISHA WATEJA WAKE MSIMU WA SIKUKUU




Meneja Mauzo wa Channel wa Kampuni ya Star Times Bw.David Kisaka kushoto akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusu kuwazawadia wateja wake kwa njia mbalimbali ikiwemo simu za mkononi,fulana,mafuta ya kupikia, pamoja na mchele kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka

WAANISHI WA HABARI WAKISIKILIZA KWA MAKINI OFA ZATAKAZOTOLEWA NA STAR TIMES MSIMU HUU WA SIKUKUU ZA MWISHONI MWA MWAKA

WAANDISHI WAKISIKILIZA

WASANII KIBAO KUSINDIKIZA TAMASHA LA GURUMO TCC CLUB



Mwimbaji mkongwe nchini, Muhidin Maalim Gurumo.
BENDI za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao kutoka Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha kubwa la Gurumo 53 litakalofanyika mwezi huu.
Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidin Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu.
Kwa mujibu wa kamati ya watu sita inayoratibu tamasha hilo, Gurumo anaagwa baada ya kutangaza rasmi kuachana na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.
Mratibu wa kamati hiyo Juma Mbizo amesema kutakuwa pia na wasanii wa bongo fleva, vichekesho na sarakasi.
Aidha Mbizo amesema tamasha litatanguliwa na bonanza la soka la maveterani.

Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala, Benno Villa Anton, Tshimanga Kalala Assossa na Ibrahim Mwinchande.
Baadhi ya wasanii wengine watakaotumbuiza ni Komandoo Hamza Kalala, Kassim Mapili, Hafsa Kazinja na Waziri Ali.
Kamati ya Gurumo iko chini ya uenyekiti wa Asha Baraka, makamu ni Waziri Ali na katibu ni Said Mdoe huku mratibu akiwa Juma Mbizo, wajumbe ni Said Kibiriti na Richardson Sakala.

BONDIA OMARI KIMWERI LION BOY ASEMA YUPO FITI KUNYAKUWA UBINGWA WA DUNIA



OMARI KIMWERI KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA MTANZANIA

Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China   November 30  na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china 
xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo

Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa


na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC 


Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi  ya  mwisho ya kujiandaa na mpambano huo amesema kuwa yeye bindafsi yupo tayali kabisa kwa mpambano huo kwani yeyey pia ni bingwa na katika kuzihirisha hilo ameomba watanzania waendelee kumuombea kwani uwakika wa yeyey kunyakuwa ubingwa huo ni mkubwa sana aliongeza kwa kusema ubingwa huo baada ya kuunyakuwa atakuja nchini Tanzania ili kuwaonesha mkanda huo wa ubingwa wa Dunia mana ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote 
 huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri

HIKI NDICHO KIPAJI KIPYA ALICHOKIIBUA MWANAMUZIKI SNURA KWA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA YANGA NA TAIFA STARS MRISHO HALFAN NGASSA.



Mrisho Halfan Ngassa anavyo mbebeleza mahaba ya Snura kwa kumsuka nywele.


WAKATI hali ikizidi kuwa tete nyumbani kwa mshambuliaji wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa baada ya kudaiwa kuwa kumeibuka ugomvi mkubwa baina yake na mkewe.






Ugomvi huo unatokana na siri ya mahusiano ya mepenzi baina yake na Msanii wa Musiki wa Kizazi Kipya Snura Anton, maarufu kwa jina la majanga, msanii huyo amejitokeza hadharani na kudai kwamba hana mahusiano ya kimapenzi ya mwanasoka huyo. 


Tangu jana picha za wawili hao zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakiwa kwenye pozi mbalimbali za mahaba huku Ngassa akigeuzwa msusi wa nywele za mwana dada huyo mwenye sifa ya kurubuni wanaume, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutumia makalio yake ipasavyo wakati wowote. 


Katika maelezo yake ambayo pia yamezagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii Snura amaesema kwamba, Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo. 


“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu na alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu"; 


"Tatizo ni kwamba, simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo" Ngassa ambaye anaonekana kuwa msusi mahiri wakati mahaba akionyesha kila dalili za kuchanganywa na mahaba ya kimwana huyo. 


Hata hivyo Habarimpya.com ilimtafuta Ngassa ambaye hivi sasa yuko kwenye kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza mechi ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) lakini akashindwa kusema lolote kwa madai kwamba hivi sasa hapaswi kuzungumza chochote juu ya suala hilo. 


Mwaka 2011 akiwa katika kikosi cha Azam, Ngassa aliwahi kufumaniwa akiwa na mwanamke chumbani kwake, wakati huo akiishi katika chumba kimoja maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam, tukio hilo lilimpa fedheha mshambuliaji huyo mahiri nchini Tanzania, baada ya mkewe kupiga kelele na kualika mtaa mzima nyumbani kwake kuja kushuhudia fumanizi hilo

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF, WAJITOSA RASMI UDHAMINI WA MICHEZO



 Meneja wa LEPF Kanda ya Dar es Salaam, Amina Kassim, akikabidhi jezi kwa M-Kiti wa TUSA, Asnati Chagu. Kushoto ni mweka hazina wa TUSA, Yusuph Singo na Kulia ni Afisa Masiko wa LAPF, Rehema Mkamba.
***************************************
*MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UMEJIKITA RASMI KATIKA UDHAMINI WA MICHEZO

KWA KUANZA RASMI NA  MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA
CHAMA CHA MICHEZO VYUO VIKUU TANZANIA (TUSA)
Mfuko wa pensheni wa LAPF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania
wenye makao makuu yake Mjini Dodoma, leo umekabidhi vifaa vya michezo
vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa Chama cha
michezo cha Vyuo Vikuu vya Tanzania TUSA,  kwa ajili ya mashindano ya
TUSA yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 10 - 17 Desemba,
2013.
Sherehe fupi ya makabidhiano, imefanyika leo, katika Ofisi za LAPF,
zilizoko Milenium Towers hapa jijini Dar es Salaam, ambapo Meneja wa
LAPF Kanda ya Dar es Salaa, Bibi Amina Kassim, amesema Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umekuwa pia ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii
katika kusaidia sekta mbali mbali kama elimu, hospitali, vituo vya
kulea watoto yatima na pia katika sekta ya michezo kusaidia kuinua
michezo nchini.
Bibi Kassim amesema, hii ni mara ya tatu kwa LAPF kudhamini mashindano
kwa mara ya kwanza LAPF ilidhamini mashindano ya mwaka 2011 na 2012,
ambapo LAPF imetoa vifaa hivi kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi wa
taasisis hizo kama wanachama wetu watarajiwa.
Amesema kufuatia LAPF kuwa Mfuko bora wa Pensheni kwa kudhihirishwa
kwa tuzo iliyotolewa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii SSRA
kuwa LAPF kuwa ni  Mfuko wa Pensheni unakua kwa kasi Zaidi nchini.
Na kitendo cha LAPF kuwa imekuwa ikipata tuzo kutoka kwa bodi ya
wahasibu nchini NBAA kwa kuwa Mfuko wenye Hesabu Bora za mwaka kwa
miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008, 2009, 2010 na 2011, LAPF
sasa imeamua kujikita kudhamini michezi, ili kurudisha kwa jamii,
sehemu ya mafanikio hayo.
Akishukuru kupata vifaa hivyo, Mwenyekiti wa TUSA Taifa,  Asnati Chagu
aliishukuru LAPF kwa msaada huo, na kusema umekuja wakati muafaka, ila
pia akaomba wafadhili wengine wazidi kujitokeza ili kufanikisha
michuona hiyo.
Amesema msaada huoi wa jezi ni moja tuu ya mahitaji, lakini bado kuna
mahitaji mengine yanahitajika vikiwemo vikombe na zawadi kwa washindi
mbalimbali

P –SQUARE WATETA NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, WATEMBELEA NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO WALEMAVU DAR




Wanamuziki kutoka Nigeria, Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
  Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
 .Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea  mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi  na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.

Wednesday, November 20, 2013

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI






VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD  ZA MAFUNZO SASA  ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania



VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD  ZA MAFUNZO SASA  ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

RONALDO AIPELEKA URENO BRAZIL KWA HAT TRICK, UFARANSA NAYO YAFUZU




MSHAMBULIAJI wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameipeleka timu yake katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 baada kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sweden.
Mchezo huo ambao uliwakutanisha mastaa wawili ambao ni manahodha wa timu hizo, Ronaldo anayeichezea Real Madrid na Zlatan Ibrahimovic anayekipiga katika timu ya PSG ya Ufaransa wote walikuwa wanawania nafasi ya kucheza fainali hizo pamoja na timu zao.
Ronaldo ambaye ndiye mfungaji wa bao la pekee katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita nchini Ureno, alifunga bao la kwanza dakika ya 50 kabla ya Ibrahimovic kusawazisha dakika ya 68.
Ibrahimovic aliongeza bao la pili dakika ya 72 lakini dakika tano baadaye Ronaldo alimaliza matumaini ya Sweden kucheza fainali hizo mwakani baada ya kufua bao la pili. 

Wakati Sweden wakisaka bao la kuongoza ili wafufue matumaini ya kucheza fainali hizo, Ronaldo alizima kabisa ndoto hizo baada ya kupachika bao la tatu dakika ya 79 na kufanya mchezo huo umalizike kwa jumla ya mabao 4-2.
Nayo ufaransa imefanikiwa kutinga katika fainali hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wake dhidi ya Ukraine shukrani mabao ya Mamadou Sakho dakika ya 22, Karim Benzema dakika ya 34 na bao la kujifunga na Oleg Gusev dakika ya 72. 


Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga katika fainali hizo ni Ugiriki ambayo ilitoka sare na Romania ya mabao 1-1 lakini imefuzu kwa jumla ya mabao 4-2, wakati Croatia nayo wamepenya katika hatua hiyo baada ya kuifumua Iceland mabao 2-0.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKUU WA MSAFARA NA MWAKILISHI WA SULTAN WA OMAN, SAID ASAAD BIN TARIQ AL SAID, NCHINI KUWAIT.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwakilishi wa Sultan wa Oman, ambaye pia ni Mkuu wa Msafara wa Oman, Said Asaad Bin Tariq Al Said,  wakati walipokutana faragha jana Nov 19, 2013,  nchini Kuwait katika mkutano wa tatu wa Afro-Arab, unaomalizika leo nchini Kuwait.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwakilishi wa Sultan wa Oman, ambaye pia ni Mkuu wa Msafara wa Oman, Said Asaad Bin Tariq Al Said,  baada ya mazungumzo ya faragha walipokutana jana Nov 19, 2013, katika mkutano wa tatu wa Afro-Arab, unaomalizika leo nchini Kuwait.

BAADA YA KUPATA UBUNGE BONDIA Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ SASA ATAMANI URAIS



Klitschko: Nina kiu ya Ikulu
MIAKA ya hivi karibuni wanamichezo na wasanii nchini ikiwamo na wale wa nje ya nchi wamezinduka wakijitosa kwenye masuala ya kisiasi kama udiwani, ubunge, ugavana na hata ngazi ya juu ya urais. 
Leo katika maisha ya wenzetu tutaangazia maisha ya ya mbabe Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ bingwa wa uzito wa juu wa WBC, aliyetangaza azma yake kuwania urais wa nchini Ukraine katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Katika taarifa yake na wanahabari anasema: “Nahitaji kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hakuna anayeweza kunizuia kugombea,”
Klitschko (42), anasema: “Ingawa nimekuwa nikiishi nchini Ujerumani, kwangu naona hilo si tatizo la kunizuia kuwania urais wa nchi hiyo kwa mujibu wa Katiba kwani ninabaki kuwa raia wa Ukraine.”
Mbabe huyo yuko katika rekodi ya wababe wa uzito wa juu wanaotambuliwa na WBO kwa kufanikiwa kutwaa mikanda mitatu ya ubingwa wa dunia, wengine wakiwa Muhammad Ali, Evander Holyfield na Lennox Lewis.
Usichokijua
Mbabe huyo mwaka 2006 aliwahi kuwania umeya wa Kiev lakini alijikuta akibwagwa na mwaka 2008 alifanikiwa kutwaa umeya wa halmashauri ya Kiev.
Mwaka jana alifanikiwa kuwa mbunge wa Bunge la Ukraine kupitia chama cha UDAR.
Mwaka 2005 wakati akimchapa Hashim Rahman na kutwaa ubingwa wa WBC alitangaza kustaafu mchezo huo,  lakini Januari 24, 2007 alitangaza kurejea upya.
Ndiye mbabe ambaye anatarajiwa kubadili mawazo ya Lenox Lewis ya kustaafu, kutokana na hivi karibuni Lewis kutangaza kwamba iwapo atatokea mdhamini mwenye dola milioni 100 za kumlipa ataingia kucheza na Vitali.  
Mahusiano
Mbabe huyo na mkewe Natalia Egorova aliyekuwa mwanariadha na mwanamitindo wamebarikiwa kuwa na watoto watatu ambao ni Yegor (Daniel), Elizabeth (Victoria) na Max.
Utajiri
Mbabe Vitali Klitschko anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 65; fedha ambazo nyingi zake amezipata kupitia masumbwi, siasa na nyingine katika matangazo ya kampuni ya Ambergo na kampuni ya Shiatzy Chen na kuna wakati alikuwa akivaa nguo ya chini yenye nembo ya D-Star 200.
Vyakula
Mbabe huyo anatumia kiasi cha dola 20 kwa siku kwa ajili ya chakula anachokuwa anakula. Ikiwa ni kaa, mbogamboga na vingine vyenye asili ya Ukraine.
Usafiri
Ana magari kama Cadillac Escalade alilonunua kwa dola 75,000 na pia anayo nyingine inayokwenda kwa jina la 4Porsche Carrera GT aliyonunua kwa dola 440,000.
Nyingine ni Lexus LS 460 Sedan alilonunua kwa dola 60,000. Mercedes-Benz S65 lilomgharimu dola 210,000.
Jengo
BONDIA huyo anamiliki jengo lake katika maeneo ya Berlin, Ujerumani, likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 11.
Jengo lake jingine liko Ukraine likiwa katika maeneo ya Kiev likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 5.
Mawasiliano
Kwa masuala ya mawasiliano ya mwanamasumbwi huyo unatakiwa kutembelea website yake ambayo ni www.klitschko.com/vitali.
Wasifu
JINA: Vitali Volodymyrovych Klychko
UZITO: Futi 6 inchi 7
TAIFA: Ukraine
UMRI: 42
Makala hii imeandaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mitandao.

Sunday, November 17, 2013

YASSIN ABDALLAH AJITOKA KATIKA TUZO BAADA YA KUKOSEKANA KWA JINA LA SUPER D KWENYE ORODHA


YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO                               
           taarifa rasmi-vyombo vya habari-michezo.
                       yah;- kujiondowa kuwania TUZO ya boxing award

ninayo hashima kwenu kuwafahamisha yafuatayo;

hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ambazo zimetolewa na watu wenye nia njema kabisa ya kutaka kuuenzi mchezo wetu wa masumbwi ya kulipwa na ya ridhaa kwa kujaribu kuwapatia TUZO wanamasumbwi [mabondia] wa pande zote mbili.

lakini inaelekea wale ambao walipelekewa wazo hili hawana nia njema ya kutaka jambo hili lifanikiwe.


kwani kabla ya hata kura zenyewe kuanza kupigiwa washindani ofisi zetu za TPBO tumekuwa tukiletewa malalamiko kutoka kwa baadhi ya mabondia ambao wameachwa kuorodheshwa nan hata wadau wengine pia wameachwa na kuingizwa watu ambao hawastahili ,huu ni ubaguzi ambao sidhani kama ni lengo la waandaaji wa TUZO hizi,.niewasilisha malalamiko hayo kwa wahusika ,nao wanarushiana mpira kwamba ni kiongozi wa juu wa pst ameondowa baadhi ya majina waliyoyaweka katika orodha.


niejaribu kusoma kwa undani sana orodha ya majina ambayo nimetumiwa  ya wanaoshindanishwa katika TUZO hizo,wamo waandishi wa habari ambao TPBO inadhani wana haki ya kupewa tuzo bila kushindanishwa kwa kuwa wao ndiyo wameufanya mchezo wa masumbwi kujulikana sana miaka hii baada ya kuzimia kwa miaka takribani 7 ya nyuma kutokana na viongozi wabinafsi , ambao bado wanataka kuuingiza katika TUZO hizi.


mfano unapoyaandika majina ya watangazaji wa chombo kimoja cha habari [TV REDIO AU GAZETI na ukamuacha mmoja wao kushindania TUZO hii je huoni kama huutambuwi mchango wake ,na tayari umeshajenga matabaka kazini kwake?


nimeshtushwa sana nilipoliona jina langu la yassin abdallah ustaadh,limo kwenye kuwania tuzo ya kiongozi bora,halafu naangalia wanowania tuzo kwa upande wa waamuzi na majaji sioni jina la referii au jaji hata mmoja  kutoka TPBO ina maana hao waliowasaidia waandaaji kuwapatia majina hawawajuwi waamuzi wa tpbo au ndiyo ubaguzi?


nimeangalia pia katika 0rodha ya waandishi sijaliona jina la SUPER D COACH [Rajabu Mhamila]
  ambaye ana miliki mtandao wa habari za masumbwi wa  www.superdboxingcoach.blogspot.com  
mtandao huo umekuwa ukitujuza habari mbalimbali za masumbwi za ndani na nje ya nchi hii

bado najiuliza tena hivi hao waliowasaidia waandaaji wa TUZO hii hawamjuwi SUPER D COACH au hii TUZO imeshafanyiwa hila za kuwatenga watu muhimu katika BOXING? NANI ASIYEJUWA MCHANGO WA SUPER D KATIKA NGUMI ZA KULIPWA,NA NGUMI ZOTE KWA UJUMLA HAPA, NCHINI TANZANIA ? MPAKA ASAHAULIWE KIASI HIKI


KWA MAELEZO HAYA PEKEE INAONYESHA NI JINSI GANI WATU WANAOJIITA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAVYOTAKA KUVURUGA DHAMIRA NJEMA YA WAANDAAJI WA TUZO HIZI KWA KUWABAGUWA WATU KWA CHUKI BINAFSKI.


UAMUZI WANGU BAADA YA HAYO YOTE NINALIONDOWA JINA LANGU RASMI KUWANIA TUZO HIZI PAMOJA NA SABABU ZIFUATAZO;-


[A]TPBO-LIMITED NI KAMPUNI KUBWA [search google] NA MIMI PIA NINAYO HESHIMA KUBWA KWA WATANZANIA KWA KAZI NINAZOWAFANYIA ,HIVYO SIKO TAYARI KUSHINDANISHWA KATIKA TUZO AMBAZO HAZINA VIGEZO VYA KUSHINDANIA.


[B] TPBO-LIMITED SIYO MIMI PEKE YANGU BALI NI PAMOJA NA WAAMUZI NA VIONGOZI WENGINE PIA.


[C] TPBO-LIMITED HAIKO TAYARI KUONA WATU WANATUMIA FURSA HII YA TUZO KUPENDEKEZA MAJINA KWA LENGO LA KUWABAGUWA WENGINE KWA FANI MOJA WAZIFANYAZO NA ZINAZOFANANA.KWA SABABU ZISIZOELEWEKA.


[D] TPBO-LIMITED INAHESHIMU SANA WAZO LA WAANDAAJI WA TUZO HIZO, LAKINI HAIHESHIMU KABISA MFUMO ULIOTUMIWA NA VIONGOZI WA NGUMI WALIOPENDEKEZA MAJINA YA MABONDIA NA WADAU WENGINE ,KWANI YANAANZA KULETA MALUMBANO YASIYO YA LAZIMA.


[E]TPBO-LIMITED BILA KUBAGUWA ITAWAPATIA HATI WADAU WOTE WALIOACHWA  KWA CHUKI BINAFSI AKIWEMO SUPER D COACH KWA KUTAMBUWA MICHANGO YAO MIKUBWA WALIYOITOWA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA.

                                AHSANTENI SANA                              IMELETWA KWENU NAMI                     YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO

MABONDIA WA TANZANIA WACHEZEA VICHAPO RUSSIA


Ramadhani Shauri
MABONDIA waenderea kuchezea vichapo nje ya nchi ambapo bondia

Ramadhani Shauri kapigwa na Roman Andreev wa Russia kwa k,o raundi ya 7

na Nassibu Ramadhani kapigwa na Nikolay Potapov kwa point

na Thomas Mashali kachezea kichapo kutoka kwa Arif Magomedov wa Russia ko ya raundi ya pili

na bondia Alphonce Mchumiatumbo alipata kipigo kutoka kwa Ruslan Semenov raundi ya 4

Saturday, November 16, 2013

KIKUNDI CHA CEPA CHATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA MSIMBAZI



Wanachama wa kikundi cha  kuondoa umasikini cha Ukonga ' CEPA' wakiwa wamebeba vyakula walivyopeleka katika kituo cha watoto yatima cha Msimbazi mwishoni mwa wiki iliyopita kikindi hicho kilitoa vyakula mbalimbali vikiwemo unga,mchele,sukari, mafuta maharage na baadhi ya vitu mbalimbali
Mwenyekiti wa kikundi cha wanachama cha kuondoa umasikini Ukonga 'CEPA' ,Ipyana Kibona kushoto na Katibu mkuu wa kikundi hicho, James Musokwa wakisukuma bembea walipo tembelea watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kutoa vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto hawo yatima
Mwenyekiti wa kikundi cha wanachama cha kuondoa umasikini Ukonga 'CEPA' ,Ipyana Kibona kushoto na Katibu mkuu wa kikundi hicho, James Musokwa wakisukuma bembea walipo tembelea watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kutoa vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto hawo yatima
Wanachama wa kikundi cha  kuondoa umasikini cha Ukonga ' CEPA' wakisukuma bembea watoto yatima wa kituo cha msimbazi walipotembelea na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto hawo yatima
Mwenyekiti wa kikundi cha wanachama cha kuondoa umasikini Ukonga 'CEPA' ,Ipyana Kibona akimkabidhi mtoto yatima anaelelewa katika kituo cha msimbazi,Baraka Mabibo msaana huo walioutoa na kupokelewa kwa niaba ya watoto wenzie

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA DKT.SENGONDO MVUNGI JIJINI DAR LEO



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Mwili ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.....
 Mwili ukuwasili kwenye Viwanja vya Karimjee.....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akilishwa Sakrament wakati wa shughuli hiyo kwenye Viwanja vya Karimjee.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Jaji Warioba,akizungumza wakati wa shughuli hiyo....
 Meza kuu ya wachungaji walioendesha shughuli hiyo...

SERIKALI KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 219 KUJENGA GATI 4 KATIKA BANDARI YA MTWARA



Na Fatma Salum-Maelezo
Serikali kutumia takriban  dola za marekani milioni 219 kujenga  gati 4 katika bandari ya Mtwara ambapo tayari taarifa ya upembuzi yakinifu imekamilika.

Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi Uwekezaji na Uwezeshaji  toka Ofisi ya Waziri Mkuu John Mboya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Akieleza zaidi  John amesema mradi huo ni matokeo ya utekelezaji wa kanuni za Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ya mwaka 2011 ambapo sektabinafsi inahusikanakukarabati,kujenga,kuendesha,kutunza au kusimamia mradi mzima.

Akifafanua zaidi John amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia idara yake imeendaa mafunzo kwa maofisa 60 walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya DPP.

Akitolea mfano alisema Serikali inaweza kuwa na mkataba na muwekezaji katika mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa  km 100 wenye viwango Fulani ambapo muwekezaji atatakiwa kusanifu, kujenga na kuendesha kwa gharama zake na hatimaye baada ya kurudisha mtaji wake na faida,anakabidhi mradi huo serikalini.

Alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa barabara ya Dar es salaam-chalinze (km 100)kuwa barabara ya haraka (Expressway)ambapo wakala wa barabara umekamilisha hatua za awali za upembuzi yakinifu wa awali.

Mradi mwingine ni ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo na eneo huru la biashara ambapo Serikali inashirikiana na mwekezaji kutoka China, ambapo majadiliano na mwekezaji yanaendelea ili mradi huu ulete tija kwa Taifa.

Kilimanjaro Stars yapangwa mchekea Chalenji Cup 2013





BARAZA la Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linatarajia kutangaza ratiba rasmi ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika nchini Kenya. tayari makundi ya michuano hiyo yametangazwa.
Tanzania Bara inayowakilishwa na Kilimanjaro Stars yenyewe imepangiwa kundi mchekea la B pamoja na timu za Zambia ambao ni waalikwa, Burundi na Somalia.
Wawakilishi wengine wa Tanzania, Zanzibar Heroes ya Zanzibar yenyewe imepangwa kundi A na wenyeji Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini, wakati kundi la kifo ni kile la C lenye timu za Uganda ambao ni mabingwa watetezi , Rwanda, Sudan na Eritrea.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia Novemba 27 jijini Nairobi kuwania taji hilo ambalo kwa miaka mingi limetawaliwa na Waganda.
MAKUNDI YALIVYO CHALENJI 2013:
KUNDI A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan

KUNDI B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia

KUNDI C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.

Kaseba, Segu wapigwa kwa KO Australia


 http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/06/Kaseba.jpg
BINGWA wa taifa wa ngumi za kulipwa nchini, Japhet Kaseba usiku wa kuamkia leo amekumbana na kipigo cha KO ya raundi ya pili toka kwa mwenyeji wake, Jeremy van Diemen katika pambano la kimataifa la uzito wa Light Heavy lililochezwa nchini Australia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa, Mtanzania hatua huyo hakuweza kuhimili makali ya mpinzani wake na kukubali kipigo cha KO ya raundi ya pili tu ya mchezo huo uliokuwa uwe wa raundi sita uliochezwa kwenye ukumbi wa Metro City.
Inaelezwa Kaseba anayefahamika kama Champion, alionyesha upinzani katika raundi ya kwanza tu, kabla ya kushindwa kuhimili ngumi nzito za mpinzani wake ambaye katika mapambano saba aliyocheza sasa ameshinda matano manne kati ya hayo ni ya KO).
Kabla ya Kaseba kudundwa, bondia mtanzania mwingine,m Jonas Segu naye alikumbana na kipigo kama hicho cha KO baada ya kunyukwa na Luke Sharp katika pambano la utangulizi uzito wa kati.
Segu alishindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 5 raundi moja kabla ya kuhitimisha pambano hilo na kuendeleza unyonge wa mabondia wa Tanzania wanapoenda kucheza nje ya nchi kwa kupigwa kila mara.
Mabondia hao wawili wanatarajiwa kurejea nchini kesho kinyonge.

Thursday, November 14, 2013

SALHA ISRAEL ATEMBELEA KAMBI YA TANZANIA TOP MODEL 2013




 Salha israel mrembo alieng'ara miaka ya 2011 katika mashindano ya urembo nchini,akiongea na washiriki wa Tanzania Top Model 2013 namna ya kujiamini wakiwa katika jukwaa na kujibu maswali endapo watakabiliana na vyombo vya habari.


Washiriki wakimsikiliza kwa makini Salha Israel wakati akiongea nao.
 Washiriki wakiwa katika picha ya paoja na Salha israel.
   Salha Israel.
 Sahaa  and friends.
 Catwalk..one two..one two.