Bondia Pendo Njau kulia akiwa amepozi na mtoto wake siku ya kushudia mpambano wa Maneno Osward na Rashid Matumla
Wednesday, February 29, 2012
BONDIA WA KIKE PENDO NJAU AJIFUNGUA SALAMA AWASHUKURU WADAU KWA KUMUOMBEA DUWA
Bondia Pendo Njau kulia akiwa amepozi na mtoto wake siku ya kushudia mpambano wa Maneno Osward na Rashid Matumla
MSONDO NGOMA YAMNYAKUA SHABANI LENDI WA SIKINDE
Kiongozi wa bendi ya Msondo, Saidi Mabela (kulia) akimkabidhi Saxaphone msanii mpya wa bendi hiyo Shabani Lendi Dar es Salaam leo, baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili akitokea bendi ya Sikinde katikati ni Meneja wa bendi hiyo Saidi Kibiliti.(picha na www.burudan.blogspot.com)
SIMBA KUZINDUA TELEVISHENI YAKE
TPBC KUANZISHA TAASISI YA RASHID MATUMLA SPORTS ACADEMY

Katika juhudi za kuwaenzi wanamichezo walioliletea sifa kubwa taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) iko kwenye mchakato wa kuanzisha Taasisi ya Michezo ya Rashid Matumla (Rashid Matumla Sports Academy) ya kuibua vipaji vya vijana wanaochipukia katika michezo hususan ngumi.
Huu ni mkakati wa kumwandaa bingwa wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (Rashid Matumla) kustaafu ngumi ili aweze kutumia kipaji chake cha ngumi kuendeleza vijana.
TPBC inajivunia historia nzuri ya Rashid Matumla kwa kuwa bondia wa kwanza Tanzania kuwa bingwa wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) pamoja na sifa kemkem alizoliletea taifa hili kipindi hiki chote anachopigana ngumi. Tunapenda kuutangazia umma kuwa tunamwandalia Rashid Matumla mazingira mazuri ya kustaafu ngumi.
Katika taasisi hiyo ya Rashid Matumla Sports Academy, Rashid atakuwa ndiye Rais na atakuwa analipwa mshahara kama mwajiriwa kwa kipindi chote cha uhai wa taasisi hiyo na kumfanya aweze kujipatia ajira ya kudumu wakati hachezi tena ngumi. Huu ni moja ya mikakati ya TPBC kuhakikisha kuwa mabondia wake walioiletea nchi hii heshima kubwa wanaenziwa kwa kuandaliwa maisha mazuri wanapostaafu ngumi!
Ni lazima kama taifa tuwajali wale wote wanaolipigania taifa hili na tutaendelea pia kuandaa mazingira mengine ya kuwawezesha waishi vizuri na kuheshimiwa daina ili kuleta changamoto kwa wengine ili nao wapigane kufa na kupona kuliletea sifa taifa letu katika michezo.
Taasisi hii itazinduliwa rasmi wakati wa mpambano wa Rashid Matumla na Vitaly Shemetov bondia anayetoka Urusi litakalofanyika mjini Moshi tarehe 22nd Juni na kuhudhuriwa na Mcheza sinema maarufu wa Marekani, Deidre Lorenz wa sinema maarufu ya Santorini Blue. Mcheza sinema huyo atakuwepo nchini kwa ajili ya kukimbia mbio za Marie Frances Mt. Kilimanjaro Marathon kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika zikazofanyika tarehe 24 Juni mwaka huu kuanzia Moshi Club.
Taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy ambayo itakuwa inafanya kazi nchi nzima itajumuisha pia bingwa mwingine wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) Magoma Shaban. Hawa wote watakuwa waajiriwa wa taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy wakifanya kazi za kuibua vipaji kwa vijana Tanzania nzima!
MEDIA DAY 2012 KUFANYIKA MACHI 24 MSASANI BEACH

WW.BURUDAN.BLOGSPOT.COM YAMTAKIA HAPPY BIRTHDAY NJEMA JOHN BUKUKU WA FULL SHANGWE!
WWW.BURUDAN.BLOGSPOT.COM INAUNGANA NA WADAU WENGINE WA HABARI NCHINI KUMTAKIA HAPPY BIRTHDAY NJEMA MWANA LIBENEKE MWENZETU JOHN BUKUKU MMILIKI WA FULLSHANGWE BLOG KWA KUTIMIZA MIAKA KADHAA YA MAISHA YAKE.
KWA NIABA YA WADAU NA MASHABIKI WOTE WA BLOG ZA BURUDAN,VIWANJANI,MACHELLAHM NA SUPERDBOXINGCOACH TUNAKUTAKIA MAISHA MEMA NA YENYE FURAHA WEWE PAMOJA NA FAMILIA YAKO KAKA MKUBWA. ALUTA CONTINUA FULL SHANGWE! INAENDELEA MANA UMEKUA MDAU MKUBWA WA KUPASHANA HABARI
Tuesday, February 28, 2012
WASHINDI WA SHINDANO LA ZAMU YAKO KUSHINDA WA KAMPUNI YA TIGO WAZAWADIWA
akikabidhi zawadi kwa mshindi wa lap top ,Flora Lyimo baada wa kuiibuka mshindi
wa promosheni ya zamu yako kushinda anaeshuudia katikati ni Mratibu wa
Promosheni na Matukio wa Kampuni ya tigo,Edward Shila
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAADHIMISHA SIKU YA WADAU KWA KUTOA MSAADA WA MASHUKA 700 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI MBEYA
Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee, akitoa msaada wa Mashuka kwa Mganga
Mfawidhi wa
Kituo cha Afya cha Ruanda kinachotoa huduma kwa kinamama
Wajawazito, Eliot
Sanga, wakati ujumbe huo ulipofika katika kituo hicho
kukabidhi misaada
msaada huo leo Jijini
Mbeya.
wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NHIF, Mariam More, akikabidhi sehemu ya mashuka kwa
ajili ya
baadhi ya Wodi za Hospiali hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano
hayo
iliyofanyika leo jijini Mbeya. Jumla ya Mashuka 700 yalikabidhiwa
katika
hafla hiyo leo.ANAYEPOKEA KATIBU WA AFYA WA HOSPITALI HIYO BI
DORICE
NZIGIRWA
wa Bodi ya Wakurugenzi
wa NHIF, Mariam More (kushto) akitandika moja ya shuka
katika kitanda
kilichopo Wodi ya Wazazi kwenye Hospitali ya Igawilo baada ya
kukabidhi
msaada wa mashuka.ANAYEMSAIDIA NI NESI MWANDAMIZI BI
DORICE
MWAKABENGA.
si Mume Bwege bali ni mume
anayeelewa majukumu ya Familia vilivyo, huu ni mfano
bora kwa wanaume
ulioonyeshwa na kidume huyu aliyejulikana kwa jina la Gibson
Mwalibwa, akiwa
na mtoto wake mgongoni wakati akitoka kupata huduma ya afya
katika kituo
hicho
Monday, February 27, 2012
MASHINDANO YA SAFARI RAGER NYAMA CHOMA
AIRTEL YAWAZAWADIA WASHINDI WA “NANI MKALI” PROMOSHENI
· Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki wazawadi
Waziri Tibaijuka akabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya NBC Lady Captains’’ Trophy 2011.





TRA YAANZISHA MPANGO MPYA WA UKUSANYAJI KODI
Ujio wa kipindi kipya cha TV "Ongea na Janet Tv Talk Show."!
Janet akirekodi kipindi na mmoja wa wadau wake aliyefika studio

Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV Talk Show pichani kulia akiwa na mmoja wa wadau akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.
Ongea na Janet ni Talk show ambayo inazungumzia mambo yanayotugusa katika maisha yetu ya kila siku,Inahusisha Jinsia zote na rika zote. Kipindi changu nilikitengeneza mwaka 2009 june 26 lakini bahati mbaya ilikuwa ni ngumu sana kupata airtime hasa ikizingatiwa ni kipindi toka nje ya kampuni husika,bado wahusika hawajakubali kubadilika ila hii "ishu" digital itasaidia sana. -Sijaajiriwa na Clouds Tv bali tumeingia Mkataba kama (partiners) .
Ni kipindi ambacho sitegemei kishuke bali kitakuwa kinapanda na watu wategemee mabadiliko,nimeanzia chini napanda juu katika kuleta changamoto,Natamani watu wenye talents wazitumie bila kuogopa na wasikate tamaa,kwa mfano,nimehangaika na kipindi changu kwa miaka mitatu na sasa ndio naanza kuona matunda ya uvumilivu,ubishi wa kutimiza ndoto na kutokukubali kushindwa kufikia malengo.
Wasijali maneno ya watu ya kukatisha tamaa,mtu asimame kwenye anachokiamini na akifanyie kazi haijalishi itachukua muda gani.Nategemea,kuelimisha,
Sunday, February 26, 2012
MSONDO NGOMA YAFANYA MAKAMUZI UKUMBI WA MAX BAR LEO
Wasanii wa bendi ya msondo wakitumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kushoto ni mpiga gita la RIDHIM, Mustafa Pishuu na mpiga tumba Amiri Said Dongo.(Picha na www.burudan.blogspot.com)
Waimbaji wa Bendi ya Msondo ngoma Baba ya Muziki wakitoa burudan wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kushoto ni Shabani Dede na Juma Katundu.(Picha na www.burudan.blogspot.com)
MBIO ZA VODACOM 5KM FUN RUN ZAFANA NDANI YA KILI-MARATHON MJINI MOSHI

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha kuanzia 20,000/= kwa mshindi wa tatu upande wa wanawake Natalia Elisante, wa mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.






MASHINDANO YA NBC LADIES GOLF SECTION YAFANYIKA LEO GYMKANA CLUB
Saturday, February 25, 2012
MATUMLA AMSAMBALATISHA MTAMBO WA GONGO
Refarii Antoni Luta katikati akimnyoosha mkono juu bondia Rashidi Matumla Snake Man kuashiria ushindi dhidi ya mpinzani wake maneno Osward Mtambo wa Gongo kushoto wakati wa mpambano wao uliochezwa Jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Matumla alishinda kwa point.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/
Date: 2012-02-25Venue: PTA Hall, Dar es Salaam , TanzaniaCommission: Pugilistic Syndicate of TanzaniaPromoter: Issa Malanga Promotion [1] Lightfly weight Moses Musa WPTS 4 rounds of a 4 rounder VS Fred Cloud- Referee: Ramadhan Basta 39 - 37 [2] Super Featherweight 6 roundsShomari Mirundi DREW 4 rounds of a 4 rounder VS Mohammed Kashinde- Referee: Pembe Ndava 38 - 38 [3] Super Bantamweight 4 roundsMuhidini Ndolanga WPTS 4 rounds of a 4 rounderVS Shukuru Said- Referee: Ramadhan Basta 40 - 36 [4] Light Welterweight Hamis Mputeni WKO round 2 of a 6 rounder VS Rashid Makali- Referee: Pembe Ndava; Judges:Ramadhan Basta, Emmanuel Mlundwa, Anthony Ruta [5] Flyweight 6 roundsHassani Kiwale WTKO round 2 of a 6 rounder VS Mawazo Kanju- Referee: Emmanuel Mlundwa Judges: Pembe Ndava , Ramadhan Basta, Anthony Ruta [6] Super Middleweight 6 roundsIdd Kigula WTKO round 4 of a 6 rounder VS Shabani Kaineko- Referee: Emmanuel Mlundwa Judges: Pembe Ndava , Ramadhan Basta, Anthony Ruta [7] Female Boxing Middle/Super MiddleMonica Mwakasanga WPTS 4 rounds of a 4 rounder VS Furaha Nganda - Referee: Emmanuel Mlundwa 40 - 36 [8] Super Middleweight 10 roundsRashid Matumla WPTS 10 rounds of a 10 rounder VS Maneno Oswald- Referee/Judge: Anthony Ruta 97 - 93; Judges: Pembe Ndava 95 - 95, Ramadhan Basta 97 – 95
RASHIDI MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA LEO FEBRUARY 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR...!!!
Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa
kuwa Februar 25 mwaka huu leo yanaenda vizuri.Promota wa mpambano huo Issa
Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina
ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99
Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki.
Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja
na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.
Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati,
litafanyika kwenye ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam
Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai
alishinda katika mpambano wao wa mwisho
Aidha aliwataja wakali watakaosindikiza mpambano huo ni Shomali
Mirundi na Mikidadi Abdallah 'Tatson', na Iddy Mkenye atapambana na
Shabani Mtengela ' Zunga Boy', Abdallah Mohamedi na Saleh Mkalekwa
mbali na hayo mpambano mwingine ni Ramadhani Mashudu na Hassani Kiwale
'Moro Best
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Roy Jonas,Evander holyfield,Lenox Lewis, Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali
ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila
‘Super ‘D’.
“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
pambano la Cheka na Maugo ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’
MAMA ASHA BILAL ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA KATANDALA SUMBAWANGA



