Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 25, 2013

YANGA YAANZA NA MKONO, YAICHAPA ASHANTI 5-1 TAIFA, HUKO TABORA SIMBA 2-RHYNO 2


 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) akiwania mpira na mabeki wa Ashanti, wakati wa mchezo wa fungua dimba la Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imechabanga Ashanti jumla ya mabao 5-1.

Bao la kwanza lilifungwa na Jerson Tegete, katika dakika ya 10, bao la pili likafungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 47, na la tatu likafungwa tena na Jerson Tegete, katika dakika ya 57, la nne likawekwa kimiani na Haruna Niyonzima katika dakika ya 73 na lakufunga pazia hilo la mabao ya Yanga, liliwekwa Kambani na Nizar Khalfan, katika dakika ya 90+aliyetokea Benchi akichukua nafasi ya Jerry Tegete.
 Ni Juma Abdul Katikati ya mabeki wa Ashanti.
 Niyonzima akichanja mbuga.
 Sehemu ya mashabiki wa Ashanti
 Sehemu ya Mashabiki wa Ashanti.
 Hivi ndivyo, Haruna Niyonzima alivyowakalisha mabeki wa Ashanti na kukosa bao la wazi katika kipindi cha kwanza.
Mabeki wa Ashanti, walikaa.......

YANGA ilianza na :- Ali Mustafa 'Bartez', Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub 'Canavaro', (c) Mbuyu Twite, Athuman Idd, 'Chuji', Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Haruna Niyonzima.

BENCHI LA AKIBA:-
Deogratias Munishi, Oscar Joshua, Frank Domayo, Bakari Masoud, Nizar Khalfan, Issa Ngao na Husein Javu.

ASHANTI ilianza na:-
Ibrahim Abdallah, Khan Usimba (c), Emaanuel Kichiba, Ramadhan Malima, Tumba Sued, Emmanuel Memba, Fakihi Hakika, Mussa Nampaka, Hussein Sued, Mussa Kanyaga na Joseph Mahundi.

BENCHI LA AKIBA:- 
Daud Mwasongwe, Hussein Mkongo, Paulo Telly, Mwinyi Abdulrahim, Laurent Mugia, Peter Ilunda na Shaban Juma.

HUKO KWINGINEKO: Coastal Union, wameichapa JKT Oljolo 2-0 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mtibwa na Azam Fc, wametoshana nguvu kwa kufungana 1-1, katika Uwanja wa Manungu Morogoro, Mbeya City na Kagera Sugar wametoka suluhu 0-0, katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. Huko mkoani Tabora Simba imetoka sare ya 2-2 na Rhyno, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, JKT Ruvu imewafunga Mgambo JKT 2-0.

No comments :

Post a Comment