Kwa siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali
vya siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye
misiba ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali
hiyo pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba"
anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa
na mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa,
alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa
kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMBA PEPONI AMIN
No comments :
Post a Comment