Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, August 26, 2016

MABONDIA IDDI MKWELA NA HASHIMU CHISORA KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA WA TPBC



Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi Katikati ni kiongozi Ally Bakari 'Champion' Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Abdallah Zamba kushoto akitunishiana misuli na Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi  Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Mabondia wa kike Halima Bandola kushoto na Ester Kazabe wakitunishiana misuli kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa
Bondia Iddi Mkwela ajiojiwa na mtangazaji wa ITV Jimmy Tala baada ya kupima Uzito
IDDI MKWELA
Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa kushoto akizungumza na mabondia pamoja na makocha wao kufata talatibu za kumwandaa bondia pamoja na sheria zake wa pili kushoto ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Mabondia Hashimu Chisora na Iddi Mkwela wakitunishiana mishuli

Tuesday, August 23, 2016

BONDIA IDDI MKWELA ALIVYO MSAMBALATISHA MWINYI MZANGELA TAIFA


Mabondia Mwinyi Mzengela kushoto na Iddi Mkwela wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa point katika mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela kulia akipiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcut' uku akirudi nyuma wakati mpinzani wake akiwa kamkumbatia Mkwela alishinda kwa pointi mpambano uho wa raundi sita uliofanyika mwishoni mwa wki iliyopita katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia mahelekezo bondia Iddi Mkwela wakati wa mpambano wake na Mwinyi Mzengela Mkwela alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Refarii wa mpambano wa masumbwi nchini Pembe Ndava katikati akimnyoosha mkono juu bondia Iddi Mkwela baada ya kumshinda Mwinyi Mzengela kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
MABONDIA MWINYI MZENGELA NA IDDI MKWELA WAKIPONGEZANA BAADA YA KUMALIZIKA MPAMBANO WAO MKWELA ALISHINDA KWA POINTWA PILI KULIA NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA IDDI MKWELA AKIWA NA MASHABIKI WAKE AKISINDIKIZWA KWA AJILI YA KUENDA KUPAMBANA NA MWINYI MZENGELA
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' MBELE KULIA AKIMSINDIKIZA BONDIA IDDI MKWELA ALIEBEBWA JUU JUU

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA WILAYANI MLELE


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda wakati Waziri Mkuu, alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Majimoto wialayani MleleAgosti 23, 2016. Wapili kulia ni Mbunge wa Kavuu, Dkt.Pundeciana Kwembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati walipokutana katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,   kwenye kijiji cha Majimoto wilayani Mlele Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JANET MBENE AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI SEKONDARI YA ILEJE


 Mbunge wa Ileje , Mh Janet Mbene,akiakabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Ileje Agrey Mwahihojo kwa ajaili ya ukarabati wa madarasa

 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akikagua Mabweni ya Wasichana  ya shule ya Sekondari ya Ileje
 Mbunge wa Ileje ,Janet Mbene akisalimiana na Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ileje , Hamidu Mwabulanga

Saturday, August 20, 2016

MABONDIA IDDI MKWELA NA MWINYI MZENGELA WAPIMA UZITO KUWA SINDIKIZA SEGU NA MFAUME TAIFA


Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi MKwela kushoto na Mwinyi mzengela wakitamba mbele ya kamera  baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na Mabondia Iddi Mkwela kushoto na Mwinyi Mzengela baada ya kupima uzoto kwa mabondia hawo kwa ajili ya mpambano wao wa Agost 21 uwanja wa ndani wa Taifa kusindikiza mpambano wa Mfaume Mfaume na Yonas Segu Picha na SUPER D BOXING NEWS







Bondia Mwinyi Mzengela Akipima uzito kulia ni mpinzani wake Iddi Mkwela na kushoto ni msimamizi Ibrahimu Kamwe Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela akipima uzito

daktari wa mchezo wa masumbwi, Donald Madono kulia akimpima bondia Iddi Mkwela Afya yake kabla ya mpambano wake na mwinyi Mzengela Kesho
Picha na SUPER D BOXING NEWS
daktari wa mchezo wa masumbwi, Donald Madono kulia akimpima bondia Mwinyi Mzengela  Afya yake kabla ya mpambano wake na  Iddi Mkwela Kesho
Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Iddi Mkwela na Mwinyi Mzengela wamepima uzito na afya leo kwa ajili ya mpambano wao wa raundi sita mpambano utakao fanyika jumapili ya Agost 21  katika uwanja wa ndani wa taifa mpamba ambao ni wa kuwasindikiza
 Mabondia Jonas Segu na Mfaume Mfaume watakaozipiga kwa raundi nane uzito wa kg 66

Msimamizi wa upimaji wa uzito alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya ngumi za kulipwa nchini Habibu Kinyogoli ambaye alisimamia zoezi ilo la upimaji uzito pamoja na Afya kwa wachezaji wote watakao cheza
Pia aliwakumbusha sheria mbalimbali wawapo ulingoni kwani mchezaji anapaswa kujua na kuzingatia kanuni na talatibu za mchezo wa masumbwi nchini
Aliongeza kwa kusema  kuwa mapambano ya jumapili yatanza mapema sana ili kuwapa nafasi mashabiki waluni makwao wakapumziki wakiwa wamepata burudani tosha ya mchezo wa ngumi bila ya bighuza ya aina yoyote ili
Pia ulizi utakuwa wa kutosha katika mpambano uhu kwani mandalizi yote yamesha kamilika tunasubili tu kesho kwa ajili ya mchezo kamili
Bondia mwingine anaekuja kwa kasi kwa sasa katika uzito wa kati Shabani Kaoneka atapambana na Kivu Abdi mpambano wa raundi sita 

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Wednesday, August 10, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AJINOA KA AJILI YA MKENYA SEPTEMBA 17 NAIROBI KENYA



 Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia Vicent Mbilinyi kwa kumwelekeza kupiga ngumi zilizo nyooka wakati wa mazoezi ya bondiahuyo ya kujiandaa na mpambano wake wa septemba 17 kuzipiga na George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika Carnivore Grounds, Nairobi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akinolewa na kucha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kujiandaa na mpambano wake wa septemba 17 kuzipiga na George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika Carnivore Grounds, Nairobi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
 BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea amendelea kujinoa kwa ajili ya mpambano wake ujao dhidi ya
George Owano  wa Kenya mpambano utakaofanyika  katika ukumbi wa Carnivore Grounds, Nairobi
septemba 17
Mpambano uho wa kwanza kwa Mbilinyi utakaofanyika nje ya nchi na ni wakimataifa utakuwa wa raundi nane uzito wa kg 63.5
Bondia huyo anaenolewa na kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa yupo tayali kwa ajili ya mpambano uho kwana ana shaka kwa kuwa mbinu zote anazijua na siri ya ushindi wake itakuwa ni si vinginevyo 
ndio mana ameamua kuwa katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM kwa ajili ya kunolewa kwa mpambano uho ujao
nae kocha wa bondia huyo aliongeza kwa kusema kuwa Mbilinyi kwa saa yupo fiti kila idara kilichobakia kwa sasa ni mazoezi ya kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kuondoa uoga wa macho wakati wa mchezo
aliongeza kwa kusema Super D kuwa Mbilinyi ni bondia wake mwingine anaekwenda  nje ya nchi wa kwanza alikuwa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alienda Zambia na kufanikiwa kushinda kwa kurudi na ubingwa wa WPBF Afrika mwingine Ni mwana Dada Lulu Kayake aliyenda Afrika ya kusini na kurudi na ushindi
Hivyo mabondia wangu wote wanapokwenda nje ya nchi wa mara ya kwanza wanarudi na ushindi ndivyo itakavyokuwa kwa Mbilinyi ni wakati wake sasa

SUPER D COACH NA BONDIA VICENT MBILINYI

BONDIA VICENT MBILINYI KULIA AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI TANZANIA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BONDIA VICENT MBILINYI KULIA AKIWA NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI TANZANIA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BONDIA VICENT MBILINYI


 VICENT MBILINYI





SUPER D COACH NA VICENT MBILINYI

KOCHA SUPER D AENDELEA KUWA NOWA MABONDIA IDD MKWELA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE WA AGOST 21 TAIFA



Mabondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo Shule ya Uhuru Mkwela anajianaa na mpambano na Mwinyi Mzengela Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Iddi Mkwela jinsu ya kupiga ngumi zenye mikunjo ya chini 'Upcat' Mkwela anajiandaa na mpambano wake ujaodhidi ya Mwinyi Mzengela Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Iddi Mkwela jinsu ya kupiga ngumi zenye mikunjo ya chini 'Upcat' Mkwela anajiandaa na mpambano wake ujaodhidi ya Mwinyi Mzengela Agost 21 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddi Mkwela yupo katika maandalizi mazito ya mpambano wake wa Agost 21 utakaofanyika katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa dhidi ya Mwinyi Mzengela mpambano wa raundi sita kg 63
akizungumza wakati wa mazoezi yake anayo endelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM iliyopo Kariakoo Sule ya Uhuru
Mkwela amesema kuwa yupo fiti kwa ajili ya mpambano uho kwani kwasasa anajua mbinu mbalimbali alizofundishwa na kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na ndie anae nisimamia katika mapambano yangu kwa sasa ivyo natalajia kuonesha uwezo wa ali ya juu sana niwapo ulingoni kwani sitaki kumwangusha kocha wangu ambaye nafuata maelekezo yake kwa muda mrefu sasa
nae kocha Super D amesema kuwa mkwela yupo fiti sana kwani kwa sasa katika kambi yake mabondia wote wapo katika maandalizi ya mchezo wa masumbwi akiwemo bondia Vicent Mbilinyi anae jiandaa na mpambano wake dhidi ya George Owano   wa Kenya mpambano utakaofanyika Carnivore Grounds, Nairobi nchini Kenya September 17
katika mpambano wa mkwela wa Agost 21 kutakuwa na mipambano mingine ya mabondia mhachali nchini ambapo bondia Mfaume Mfaume atavaana na Jonas Segu mpambano wa raundi nane KG 66 
Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JULAI WAPUNGUA HADI 5.1




  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo (kulia) akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 ambao umefikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 za mwezi Juni 2016.Kushoto ni Kaimu Meneja wa wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Mwezi Julai, 2016 iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam. 

Na Aron Msigwa – Dar es salaam.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) imetangaza mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai 2016 na kueleza kuwa umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 iliyokuwepo mwezi Juni mwaka huu.

Akitangaza taarifa ya mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016.

Ameeleza kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2016 zikiwemo bidhaa za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9 huku bei zisizo za vyakula zikihusisha  ni gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni pamoja na bidhaa za gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Aidha, ameeleza kuwa pamoja kupungua huko, kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kwenye baadhi ya bidhaa umeonesha kuongezeka katika kipindi hicho hasa kwenye kama  mchele, mahindi, unga wa mahindi, vyakula kwenye migahawa na mkaa.

Bw. Kwesigabo amesema kuwa Fahirisi za Bei nazo zimeongezeka hadi kufikia 103.50 mwezi Julai, 2016 kutoka 103.47 za mwezi Juni 2016, ongezeko  ambalo limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula zile  zisizokuwa  za vyakula.

Amesema ongezeko hilo la Fahirisi linahusisha kundi la bidhaa na huduma za vyakula na vinywaji baridi, Vinywaji vyenye kilevi na bidhaa za Tumbaku, Mavazi ya nguo na viatu, nishati, maji na Makazi pamoja na Samani, vifaa vya nyumbani na ukarabati wa nyumba.

Kundi lingine linahusisha gharama za Afya, usafirishaji, Mawasiliano, Utamaduni na Burudani, Elimu, hoteli na migahawa pamoja na bidhaa na huduma nyinginezo ambazo jumla ya Fahirisi za Bidhaa hizo kwa mwezi huo zimefikia 103.50.

“Baadhi ya bidhaa zilizo sababisha kuongezeka kwa Fahirisi ni pamoja na mafuta ya kupikia asilimia 1.1, samaki wabichi asilimia 6.0, matunda asilimia 4.9, maharage makavu kwa asilimia 2.7, ndizi za kupika asilimia 1.9 na mahindi kwa asilimia 1.5” Amesisitiza Kwesigabo.

Mbali na hilo ameeleza kuwa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2016 umepungua hadi kufikia asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ya mwezi Juni 2016.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi ya 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 62 mwezi Julai 2016 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 65 ya mwezi Juni, 2016.

Aidha, hali ya Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki imeonesha kuwa nchi ya Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Julai umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.39 kutoka asilimia 5.80 za mwezi Juni, 2016, Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei uliopungua wa asilimia 5.1 kwa mwezi Julai kutoka asilimia 5.9 za mwezi Juni, 2016.

SERIKALI IMEJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI -PROFESA MBARAWA






Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Safari ikiwa inaendelea katika mabehewa na baadhi ya watendaji wa TRL gari moshi kati ya Pugu leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Safari inaendelea


Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza juu huduma ya usafiri wa reli kwa wananchi wa Pugu leo katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni leo jijini Dar es Salaam.
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mjini kwa kutumia usafiri wa gari moshi. 

Hayo ameyasema leo Profesa Mbarawa wakati wa uzinduzi wa gari moshi linalofanya safari zake kuanzia Stesheni hadi Pugu, amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45. 

Amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapungaza kama sio kumaliza kabisa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Profesa Mbarawa amesema kuwa katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo. 

Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli. 

Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali. 

Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu. 

Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa usafiri wameanza kutokana na nguvu ya serikali kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.