Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza Bw.Hassan Abbas kuwa
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali
kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa
Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu Namba 6(1)(b)
kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah
Mwambene uliofanyika tarehe 7 Machi 2016 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa
Wanahabari na Wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw
Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.
“Ninawaomba Wanahabari na Watanzania
kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe ushirikiano unaostahili katika
utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri Nape alimpongeza
Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa kujituma na
kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu na uadilifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi huyo mpya
amekubali uteuzi huo na ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu
mkubwa na ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara
ya Habari Maelezo na Watanzania kwa ujumla.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas
alikuwa ni Meneja Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais
inayosimamia Utekelezaji wa Program ya Matokeo Makubwa sasa (President`s
Delivery Bureau).
No comments :
Post a Comment