Vodacom Miss Dar Indian Ocean 2011, Stella Robert akipunga mkono kwa furaha baada ya usiku wa kuamkia leo kutawazwa kuwa Malkia wa Kitongoji hicho alipowashinda wanyane wengine 10 waliokuwa wakiwania taji lililokuwa likishikiliwa na Alice Luchiku Miss Kinondoni 2010.
Miss Dar Indian Ocean 2011, Stella Robert (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wengine wanafasi ya pili Hamisa Hassan (kulia) na Renada Apoley baada ya kutangazwa washindi katika nafasi hizo.
Show ya ufunguzi ya warembo ilikuwaa kama hivi....
Vazi la ufukweni kila mrembo alipita kivyake, pichani ni Linda Joshua akijaribu bahati yake.
Catherine Frisch nae alijitosa...
Zahra Anonina hakubaki nyuma...
Georgina Saula alihakikisha nae anarusha kete yake.....
Renada Apoley ambaye aliibuaka Mshindi wa tatu huenda hivi aliwachengua majaji....
Sabrina Abllah akipiota na kivazi chake cha ufukweni....
huyu ni Fatma Pongwa akijinadi kwa majaji na mashabiki....
Sikama Judith Emmanuel alitishwa na kina cha maji la hasha ni mbwembwe tu za kuwastua majaji.
Geneveive Lucas nae alitaka kufuata nyayo za wajina wake aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2010 lakini hakufurukuta.....
Hamisa Hassan alijaribu bahati yake na kuingia fainali na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2011.
Kama ilivyo andikwa katika maandiko matakatifu kuwa Wamwisho atakuwa wa kwanza na Wakwanza atakuwa wa Mwisho ndivyo usemi huu ulijidhihirisha baada ya Mrembi huyu aliyekuwa wa mwisho kuibuka wa kwanza.
Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel Mopangala (kulia) pamoja na warembo wenginine walioingia fainali za Miss Tanzania nao walikuwepo kushuhudia tukio hilo.
Kikosi kazi cha Clouds FM kilikuwa katika viunga vyua Mbalamwezi kama hivi ...
Meza ya majaji ilikuwa makini katika kufanya kazi yao...
Clouds tena waliwakilisha....
Burudani toka kwa rais wa Wasafi na Diamond ilipatikana na alishambulia vyema...
wadau walikuwepo nao kujionea kimwana anaenyakua taji hilo na walifurahi pale mrembo waliompa maxi kushinda...
Kamati ya Miss Tanzania ilikuwepo ukumbi wa Mbalamwezi kujionea tukio...
Elihuruma Ngowi kutoka Vodacom Tanzania alikuwepo katika safu ya wadhamini.
Hawa ni Nouma ndo waleeee wadada wa Nganga moja Ndembe ndembe waliwasha moto na kuzua gumzo walahi ilikuwa nouma..
Millard Ayo na kikosi chake toka Clouds walikuwepo...