Aliyekuwa mshambuliaji wa Klabu ya Yanga,Nsa Job, anatarajiwa kuondoka nchini kwenda nchini Sweden kwa ajili ya kufanya majaribio katika Klabu moja nchini humo inayoshiriki ligi daraja la kwanza.Akizungumza na mtandao wa Klabu ya Yanga,Job amesema tayari mipango yote imekamilika chini ya wakala wake Nyupi Mwakikosa ambaye anasimamia shughuli zote za kujiunga na Klabu hiyo.Hata hivyo Nsa Job amesema hadi sasa hajafahamishwa kikamilifu juu ya Klabu anayokwenda kufanya majaribio lakini tayari wakala wake amemhakikishia kuhusu majaribio hayo na ameeleza kuwa hata ikishindikana zipo Klabu mbili za America ya Kusini tayari amekwisha fanya mazungmzo nayoNsa amesema safari yake itakuwa ni ya tarehe 20/6/2011 anatarajia kuondoka na shirika la ndege la KLM.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment