Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, August 31, 2011

KOCHA RAJABU MHAMILA SUPER D AKIWA KATIKA MAPAMBANO YAKE KABLA YA KUA KOCHA


Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila (Super D) kushoto akitangazwa mshindi zida ya bondia Safari Berdard kipindi hicho
Super D Boxing Coach kushoto Akipambana na Rashidi Ali
Super D Boxing Coach kulia akipambana na Ajibu Salumu

NIPO MOROGORO NA MATAARISHO NDIO HAYA




Habibu Kinyogoli juu akijalibu kipande cha ulingo uho baada ya kufunga leo hii maandalizi yanaendelea

TTCL Yatoa Zawadi Za Idi Kwa Wazee Wasiojiweza Na Watoto Yatima Kilimanjaro

|


Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Said Amir Said aliyevaa suti akikabidhi zawadi za siku kuu ya Idi kwa wazee wasiojiweza na watoto yatima mkoani Kilimanjaro. Picha: Issa Michuzi

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATAKA WAISLAMU KUENDELEA KUTENDA MEMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agosti 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agost, 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Agosti 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agoost 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Na Ismail Ngayonga

Maelezo

Dar Es Salaam

MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ameitaka jamii kuungana kwa pamoja katika kuhimiza maadili mema na kukemea maovu badala ya jukumu hilo kuwaachia viongozi wa dini peke yao.

Akizungumza katika sala ya Idd El Fitri iliyoswaliwa kimkoa katika viwanja vya mnazi mmoja, Dkt. Bilal alisema jamii isiwategemee viongozi wa dini katika kupambana na maovu yanayoendelea kukithiri ndani ya jamii.

Dkt. Bilal alisema kila mwanajamii kwa upande wake anatakiwa si kuacha bali pia kukataza mambo yote mabaya. “Haitoshi kwa muumini mmoja kuwa mwema peke yake, halafu akayafumbia macho maovu yanayotokea katika jamii inayomzunguka” alisema Dkt Bilal

Kwa mujibu wa Dk. Bilal alisema Watanzania hawana budi kuona fahari pia kuyatekeleza maelekezo ya mwenyezi mungu ya kuifanya dunia yote kuwa yenye neema , kwani umahiri ameutukuza mwenyezi mungu kuwa umma bora.

Dkt Bilal pia aliwashukuru waumini wa dini nyingine kwa ushirikiano wao wa dhati kwa ndugu zao waislamu, uliyoweka mazingira mazuri katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani yaliyohakikisha waumini wa kiislamu wanatekeleza ibada yao bila ya karaha na bugudha.

“Uvumilivu huo baina ya dini na uhuru uliopo wa watu kuabudu imani ya dini yao ni vitu vinavyochangia katika kuimarisha amani, umoja na upendo katika taifa letu” alisema Dkt Bilal.

Kwa upande mwingine Dkt. Bilal pia aliwataka waislamu nchini kuendelea kufanyiana mema ikiwemo kutoa sadaka, kuswali na kufanya ibada pamoja na kuwasaidia wasiojiweza mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Akifafanua zaidi alisema si imani safi kudhani kuwa mema yanapaswa kutendeka tu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na badala ya hapo kuanza kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili.

“Napenda kuwaasa ndugu zangu waislamu kuzingatia wajibu wet

HARBOURS SOCIA; AND SPORTS CLAB WALA IDI NA WATOTO WALEMAVU


Mwenyeki wa Harbours Social Sports Clab ya Kurasini, Bw. Athumani Mkangara (Kulia) akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Zena Yahaya Sehemu ya msaada wa vyakula kwa ajili ya Sikukuu ya Idi El Fitri kwa watoto wasioona na walemavu wa shule hiyo Dar es salaam jana kushoto ni mwalimu Mkuu Bi. Anna Man'genya


Tuesday, August 30, 2011

NGUMI KUPIGWA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO





MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.

Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.

Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa Middle huku likisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania,(PST).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku katika uzito wa Fly ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.

"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.

Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia kajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuweza kuibuka na ubingwa ili aweze kuendeleza rekodi yake.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D

MABONDIA WA ZAMANI WATAKIWA KUFADHILI NGUMI





BINGWA wa Mchezo wa kick Boxing nchini Japhet Kaseba amewaomba Mabondia wakubwa kuhakikisha wanaweka na kuchangia fedha zitakazo kuwa zikitolewa kuchangia vyama vya michezo nchini wikiwemo RT na BFT.

Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili leo kwa njia ya simu Gwiji huyo wa Mapigano amesema itakuwa ni jambo zuri kwa mabondia wakubwa kutenga fedha ili kuchangia vyama vya michezo mbali mbali nchini wikiwemo vya Ngumi za ridhaa na riadha badala ya kutegemea nguvu ya serikali tu.

"Sifikili kama tukijaribu tutashindwa japo kwa kiasi kidogo kidogo tuweke mazoea ya kuchangia vyama hivi kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla kuliko kutegemea serikali tu"alisema Kaseba.

Hata hivyo Kaseba amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya All African Games ambayo yanatarajia kurindima hivi karibuni nchini Msumbiji yupo mbioni kuandaa filamu itakayo kuwa ikielezea umuhimu wa kuwekeza katika michezo.

"Lengo la hii filamu ni kujaribu kuwapa hamasa wadau kuwekeza na kuchangia michezo ila pia nataka kuwashirikisha wanamichezo mbali mbali"alisema Kaseba.

TTCL YAENDELEA KUTOA MSAADA ZAIDI KWA WAHITAJI






TTCL jana ilitoa msaada wa vyakula kwa watoto walemavu wa shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko pamoja na watoto wasiojiweza wa kituo cha SOS kilichopo kandokando ya barabara ya Sam Nujoma, Mwenge.









Msaada huu wa chakula unalenga kusherehekea sikukuu ya Idd El-Fitr pamoja na watoto hawa ambao kwa namna moja au nyingine ni kundi linalohitaji kusaidiwa na jamii inayolizunguka.







TTCL kama kampuni ya umma na ya kizalendo inajali sana jamii





inayoizunguka pamoja na matatizo yake ndio maanaimeamua kutoa msaada huo wa vyakula kwa makundi haya ya watoto wahitaji ni wazi kuwa ni jukumu letu kama TTCL, kampuni ya kitanzania kusaidia jamii.





Msaada huu kwa vikundi hivi viwili una thamani ya shilingi milio



ni Mbili (2 m/=). Niseme tu kuwa ni utamaduni wetu sisi TTCL kuwa wakarimu si tu kwa kundi hili bali hata kwa makundi mengine yenye mahitaji katika jamii ye



tu ya kitanzania.









Kuthibitisha hilo, Afisa Mtendaji Mkuu





wa TTCL ametoa msaada wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd Elfitr kule Moshi Kilimanjaro kwa vikundi vya wazee, yatima na walemavu wa viungo vya mwili.









Jumla ya vikundi vitatu vitafaidika na msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano (1.5millioni).









TTCL Inaahidi kuendelea kuhudumia jamii yetu pale kampuni inapofanya vizuri na mapato kuongezeka kwani ndio njia mojawapo ya kurudisha baadhi ya mapato kwa wateja wetu.







Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri kati ya TTCL na watanzania Tunaomba tusaidiane kupinga hujuma zozote dhidi ya mtandao na kampuni ya TTCL kwa ujumla.

Monday, August 29, 2011

STARS v ALGERIA NA TWIGA STARS KUAGWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 29, 2011
VIINGILIO STARS v ALGERIA
Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.
Taifa Stars tayari iko kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.
Wachezaji wan je waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo jioni.
Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.
TWIGA STARS KUAGWA KESHO
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.
Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.
Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
KIM AITA 30 TIMU YA VIJANA
Kocha wa timu za vijana Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.
Wachezaji walioitwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).
Wengine ni Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Sunday, August 28, 2011

MAN U YAIADHIBU ARSENAL 8-2

Man U yaifanyia mauaji Arsenal 8-2


Wayne Rooney amepachika mabao matatu peke yake wakati Manchester United ikiinyuka Arsenal kwa mabao 8-2.

Young

Young na Rooney

Danny Welbeck ndiye alifungua karamu ya magoli baada ya kuunganisha pasi ya Anderson.

David De Gea aliokoa penati iliyopigwa na Robin Van Persi, na baadaye kidogo Ashely Young kufunga bao la pili.

Rooney aliandika bao la tatu na la nne kwa mikwaju miwili ya adhabu, kabla ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati.

Nani na Park Ji Sung walifunga nao na Ashley Young kuongeza jingine.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Robin Van Persie.

Awali Manchester City waliizaba Tottenham Hotspur kwa mabao 5-1.

Edin Dzeko alifunga mabao manne, na Sergio Aguero akifunga moja. Bao pekee la Spurs lilifungwa na Younis Kaboul.

Kwingineko Newcastle United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham. Leon Best akifunga mabao yote ya Newcastle na goli la Fulham kufungwa na Clint Dempsey.

West Brom walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Stoke City. Goli hilo pekee lilifungwa na beki Ryan Shotton katika dakika ya 89.

USAIN BOLT AONDOLEWA MASHINDANO YA DUNIA


Bingwa wa dunia Usain Bolt ameondolewa katika fainaili za mita 100 mashindano ya dunia mjini Daegu baada ya kuanza mbio mapema, huku raia mwenzake wa Jamaica Yohan Blake akinyakua medali ya dhahabu.
Usain Bolt

Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt aliondolewa katika fainali za mita 100 kwa wanaume katika mashindano ya dunia ya riadha ya Daegu, Korea ya Kusini, huku raia mwenzake wa Jamaica, Yohan Blake, akipata dhahabu.

Bingwa mtetezi Bolt aliwashangaza mashabiki wengi wa riadha katika uwanja wa Daegu, alipoondolewa kwa kuanza mbio hata kabla kusikia mlio wa bunduki.

Blake aliweza kukamilisha mbio hizo kwa sekunde 9.92, akimtangulia Mmarekani Walter Dix (10.08) na bingwa wa dunia mwaka 2003, Kim Collins (10.09).

Lakini gumzo hasa ambalo linaendelea ni kumhusu Bolt, ambaye bado alitazamiwa kushiriki katika mbio za mita 200m na 4x100.

Kabla ya mbio, kama kawaida, Bolt alionekana kutulia.

Wengi watajiuliza ikiwa yaliyompata Bolt ni kufuatia sheria mpya kuanzishwa, inayohusu kuanza mbio mapema kabla mlio wa bunduki.

Kanuni hiyo ya riadha, nambari 162.7, inaelezea kwamba ikiwa mwanariadha ataanza mbio mapema kabla ya mlio huo, basi ataondolewa katika mashindano.

Kitambo, mwanariadha alisamehewa alipofanya kosa hilo mara ya kwanza, na aliondolewa katika mashindano iwapo alirudia kosa hilo mara ya pili.

Sheria hiyo mpya ilitangazwa na shirikisho la kimataifa la riadha, IAAF, mwanzoni mwa msimu wa riadha mwaka 2010.

Ijapokuwa Blake, mwenye umri wa miaka 21 alimsikitikia mwenzake Bolt, na ambaye hufanya mazoezi naye, alisema alifurahishwa sana na ushindi huo wa ghafula.

"Sidhani nina maneno ya kuelezea hayo, na ninahisi kulia machozi," alisema. "Nimekuwa nikisali kupata ushindi, na hii kwangu ni ndoto.

"Usain Bolt amekuwa akinisaida. Nilihisi nitapata ushindi kwa niaba ya Bolt."

Collins, mwenye umri wa miaka 35, na alielezea wasiwasi wake kuhusiana na sheria hiyo mpya, baada ya kupata medali yake ya shaba.

"Sidhani sheria hii ni sawa. Mambo haya hutokea na ni lazima uwape watu nafasi," alielezea mwanariadha huyo kutoka St Kitts na Nevis.

Bolt, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiwika katika mbio fupi miaka michache iliyopita, tangu alipovuma na kuandikisha rekodi katika mbio za mita 100 na 200 katika mashindano ya Olimpiki 2008 na vile vile Roma, akiandikisha muda wa sekunde 9.58 na 19.19.

Baadhi ya wanariadha wazoefu wa mbio za mita 100 walikuwa wamekosekana katika fainali hizo za Daegu, ikiwa ni pamoja na wanariadha Asafa Powell, Steve Mullings, Tyson Gay na Muingereza Dwain Chambers ambaye aliondolewa katika nusu fainali, pia baada ya kuanza mbio kabla ya mlio wa bunduki.







MAZOEZI YA KAMBI YA ILALA YANAENDELEA














Mabondia walio chini ya kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa katika mazoezi ya kukaza misuli katika ukumbi wa Amana CCM Dar es Salaam juzi






RANCIS CHEKA NA MADA MAUGO KUONESHANA UMWAMBA IDI PILI









timu ya taifa ya ngumi yapaaa




Mabondia,makocha pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini wakiangalia DVD zinazotahalishwa na Kocha wa mchezo wa ngumi timu ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala kimichezo, Rajabu Mhamila 'Super D' ayupo pichani ambazo zinafundisha mafunzo ya mchezo huo kabla ya kuondoka kwenda Msumbiji kushirika Mashindano ya 'ALL AFRICA GAME' yatakayoanza mapema wezi ujao timu hiyo ni ya kwanza kwa Tanzania kuondoka leo. (Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)














WAISLAMU WAALIKWA KATIKA SWALA YA IDD-EL-FITR VIWANJA VYA MNAZI MMOJA



Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Dar es Salaam August 26,2011 imetoa taarifa ya kuwaalika waislam wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika swala ya IDD- El- FITR inayotarajiwa kuswaliwa siku ya Jumanne 30 Aug au Jumatano 31 Aug,2011 kutegemea na Muaandamo wa mwezi katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.Pichani Skeikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Salum akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari alipokutana nao leo, (kulia) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkoa Dar es Salaam (BAKWATA) Sheikh Said Ponda na (kushoto ) Mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Shukuru Kilakala. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO),

MAMA SALMA KIKWETE ACHANGISHA FEDHA KWAAJILI YA TAMASHA LA (MOWE)



Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali Aug 26,2011 jinini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata I. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa muwakililishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania Gloria Kavishe(kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa uchangiaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) August 26,2011, Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya mfano ya watoto yatima WAMANAKAYAMA iliopo Rufiji mkoa wa Pwani, (Picha na Mwankombo Jmaa-MAELEZO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mwakilishi wa Bank ya CRDB (kulia)kwaajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 , (aug 26,2011)) jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/)
Picha na Mwankombo Juma-MAELEZO).
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya MOWE na vbaadhi ya viongozi wa meza kuu akiwepo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

EVANDER AWA PROMOTA WA NDONDI



Bingwa wa zamani wa dunia wa ndondi za kulipwa uzito wa juu, Evander 'The Real Deal' Holyfield wa marekani akiwa amewashika mijkono bondia Ruslan Chagaev wa Uzbekistan, kushoto na Alexander Povetkin wa Urusi kulia, katika siku ya kupima uzito kwa mabondia hao mjini Erfurt, Ujerumani juzi. Pambano la kuwania ubingwa wa dunia wa WBA uzito wa juu baina ya wawili hao lilitarajiwa kufanyika jana mjini Erfurt.

WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WAJIACHIA KWENYE MICHEZO



Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 leo walikutana na kushiriki michezo ya aina mbalimbali na hapa nawaletea baadhi ya michezo hiyo ukiwepo wa kuogelea. Hawa walionesha kushinda lakini baade walivutwa.
upande wa pili mambo yalikuwa hivi na timu hii iliibuka washindi. Licha ya kamba kukatika mara mbili.
furaha ya ushindi kwa timu ya wavuta kamba.
Warembo wa Vodacom walifungua dimba na kati ya timu za M Pesa na Voda Jamaa.
Hashimu Lundenga nae alishiriki katika soka na hapa akifanya vitu vyake.
Ulifika wakati wa kucheza mziki na mshindi wa hapa alikabidhiwa kitita cha 50,000/= aliyekwenda msamba aliibuka mshinda.

MTOTO WA JK APIGA GOZI NA TIMU YA TAIFA YA VIJANA YA U17



Khalfan Kikwete, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete(kushoto) akijaribu kuumiliki mpira aliposhiriki katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, kwenye Uwanja wa Karume Dar es Saalm, jana
Khalfan (kushoto) akiumiliki pia mpira wakati wa mazoezi hayo

HIKI NDIYO KIJIJI KILICHOCHOMWA MOTO HUKO TABORA


Mkazi wa Kitongoji cha Luganjo Mtoni katika Tarafa ya Usinge mkoani Tabora, Bahati Hussein (kulia), akiwa amekaa na familia yake nje ya mabaki ya nyumba yake, baada ya kuchomwa moto na askari wa wanyamapori na polisi agosti 15 mwaka huu kwa madai ya kujenga katika hifadhi. Nyumba 317 zilichomwa na watu 773 hawana mahali pa kuishi wanaishi vichakani.
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mgusa Maduhu (kulia) akiwa na familia yake baada ya nyumba yake kuchomwa moto.
Wakazi wa kijiji hicho wakiwaonesha mabaki ya baiskeli iliyoungua moto katika tukio hilo.
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE watoto wakicheza vichakani katika eneo la wazi walipopewa hifadhi na serikali ya kijiji.
Mama Mlemavu Magreth Jonas akilia wakati akihojiwa na waandishi wa habari hawapo pichani.
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliochomewa nyumba zao.
Mama akipika nje baada ya nyumba yake kuchomwa moto huku watoto wake wakisubiri chakula kiive tayari kwa mlo wa mchana.
<!--[if gte mso 9]> Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE Mkazi wa kijiji hicho Elia Mrisho akionesha mafuvu ya nguruwe wake waliochomwa moto. Nguruwe 26 waliteketea.
picha na habari kwa msaada wa blog ya http://fullshangwe.blogspot.com