MSANII wa nyota wa Afrika Mashariki, Jose Chameleone
ameamua kumgeukia Mungu na anatarajia kutoa kibao kipya cha gospel alichokipa
jina la ‘Tubonge’.
Chameleone ambaye kwa sasa anatamba na single yake
ya badilisha aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa kwa sasa
anataka kumgeukia Mungu na kwa kuanza anatoa wimbo huo ambao ni shukrani kwa
Mungu.
“Tunamuhitaji Mungu kwa wakati huu. Hasa katika
kipindi hiki cha hukumu.” Aliandika Chameleone katika ukurasa wake kuwaeleza
mashabiki wake wa muziki duniani kote.
Wimbo huo utakuwa wa pili kwa Chameleone utakuwa ni
wa pili wake kwani awali aliwahi kushirikishwa na msanii wa Zambia, Mampi wimbo
ulioitwa Nimakwanisa ambao umefanya vizuri sana barani Afrika.
No comments :
Post a Comment