
Karama anategemea kupanda ulingoni tena tarehe 20 ya mwezi wa kumi katika ukumbi wa ccm mwinjuma.Mwananyamala kuzipiga na sado philemon katika pambano lililoandaliwa na bigright promotion.akilizungumzia pambano hilo Ibrahim kamwe anaeleza kuwa maandalizi mpaka sasa yanaenda vizuri pindi yapo katika mazingira magumu kwa wale watakaocheza utangulizi wanajiandaa kiukataukata kwa ajili ya pambano hilo ambalo litakuwa na mapambano mengi ya utangulizi, ukizingatia hatujapata mdhamini wa kudhamini pambano hili ili liwe katika ubora unaotakiwa , lakini tunapambana na tutajitahidi pambano lifanyike vema tuwatie moyo hawa mabondia wanaochipukia na kuusimamisha vizuri mchezo wetu wa masumbwi.Karama na mwenzie philemon wameshasaini makubaliano ya mchezo huo na wapo katika hali nzuri ya kimchezo.
na
IBRAHIM ABBAS KAMWE
No comments :
Post a Comment