Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, October 7, 2009

TIMU YA TAIFA POOLTABLE YAINGIA KAMBINI

Katibu Mkuu wa Pool table Taifa ,Amos Kafwinga (kushoto) akizungumza na wahandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusu kuingia kambini kwa timu ya taifa ya mchezo uho jana na kupata mbambano wa kirafiki kati yao na Uganda kulia ni Katibu msaidizi wa Balozi wa Uganda Allan Tazenya.(Picha na Rajabu Mhamila)

LHRC WAKABIDHIWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Mratibu wa Jopo la Uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mtaa Imelda Urio kutoka kutuo cha sheria na haki za binadamu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kituo hicho kuchaguluwa kusimamia chaguzi mbali mbali za serikali za mitaa ambapo kituo kilipeleka maombi kwenye ofisi ya waziri mkuu tawala za na serikali za mitaa.

REAL YAZINDUA MWEZI KWA MWEZI

Meneja Msaidizi wa Biashara na Masoko wa Kampuni ya Real Insurance Amani Boma (kulia) akiuzungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo George Sithole na mkurugenzi Dr Steve K. Mworia.( Picha na Super D)
REAL Insuarance, leo imezindua rasmi bima mpya inayojulikana kama mwezi kwa mwezi. Bima hii ambayo ni yakwanza Tanzania, ipo kwa ajili ya kukidhi mahitaji muhimu ya watu binafsi, biashara na magari kwa mwezi.

ZAIN, MTV ZA TANGAZA MSHINDI WA TANZANIA WA SHINDANO LA MY VIDEO

Dar es Salaam, Oktoba 2009: MTV na Zain wamemtangaza kijana wa kitanzania Vanessa Bernard aliebuka mshindi katika shindano la tuzo za Muziki wa luninga wa afrika (MTV Africa Music Awards (MAMA) with Zain My Video contest).
Vanessa, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19- kutoka Dar es salaam, alimshinda Abel Aisaia na William Otuckall na kushinda tuzo za luninga yangu ya Tanzania (My Video title) – ilioandaliwa kusheherekea na kwawezesha waafrika wenye vipaji na wanaotaka kuwa mashuhuri kwenye soko la muziki.
Maelfu ya vijana wenye umri juu ya miaka 18s Afika nzima walishiriki katika mashindano na kuingia katika mashindano ya pili ya l My Video, yaliyozinduliwa na MTV na Zain mwaka 2008. Maelfu ya kura za SMS zilipokelewa kutoka kwa watanzania wakichagua mwimbaji wao wanaempenda na wakafikia washindani wa kwanza kumi.votes were received from music fans choosing their favourite singer before the contestants were whittled down to the final ten.
Vanessa ameshinda safari iliyolipiwa kushiriki tuzo za TV Africa Music Awards with Zain, yatakayofanyinka Nairobi Kenya tarehe 10 Oktoba 2009, na Vanessa anauwezekano wa kushida zawadi yake mwenye ya kikombe cha MAMAkatika hafla hiyo. Atashindana na washindi wnezake wengine kutoka nchi za, Ghana, Malawi, Kenya, Nigeria, Sierra Leone, South Africa, Uganda naZambia.
Kwa upande wake Vanessa alisema , ‘kwa kua katika washindi kumi wa tuzo za MAMA na washindi wengine ni ndoto yake kutimia ya kuwa mashuhuri katika muziki! Nina furaha kubwa kwa kuchaguliwa kwenda Kenya. Shukrani zangu za dhati ziwaendee Zain na MTV kwa kunipa fursa hii ya kuonyesha kipaji changu katika ulimwengu maridhawa’. Kutoka Tanzania kutakua na A.Y. na Professor Jay ni moja kati ya wasanii wengi watakao imba na kutembelea zulia jekundu pamoja na Vanessa katika tuzo hizi MAMA. Wasanii wengine watakao kuwepo ni pamoja na Akon, Wyclef Jean, Lizha James, Nameless, Blu3, the Mo Hits Allstars na Zebra & Giraffe.
MTV Africa Music Awards na Zain itaonyeshwa kwenye DStv na washarika wa mitandao wa MTV kama AIT (Nigeria), STV (Nigeria), CTV (Kenya), WBS (Uganda), TBC1 (Tanzania), TV3 (Ghana), ZNBC (Zambia) and RTGA (DRC) kuanzia tarehe 17 Oktoba 2009; pia itaonyeshwa kwenye huduma ya MTVNHD, MTV Network International’s high definition TV iliyozinduliwa mwezi Septemba 2008, na inayopatika na katika nchi 21 ulimwenguni (Argentina, Belgium, Caribbean Islands, Chile, Columbia, Denmark, Ecuador, Finland, France, Germany, Hungary, Israel, Netherlands, Norway, Poland, Russia, Sweden, Switzerland, Venezuela, Uruguay, UK & Ireland).

WANASOKA WA ENGLAND WAFURIKA KUSHANGILIA KIKAPU LONDON

Luol Deng amefurahia mafanikio nyumbani kwao kufuatia Chicago Bulls kuitoa Utah Jazz katika michezo ya mwisho ya maandalizi ya ligi kuu ya mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA mchezo uliyochezwa jijini London.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alimaliza mchezo akiwa anaongoza kwa kunyakua jumla ya pointi 18 na kuifanya Chicago Bulls kushinda kwa vikapu 102-101 mbele ya mashabiki 18,689 waliyohudhuria kutazama mchezo huo.
Hata hivyo Chicago inapaswa kumshukuru zaidi James Johnson ambaye alifanya kazi kubwa kuhakikisha inashinda.
Hii ni mara ya tatu mfululizo klabu zinazoshiriki NBA kucheza michezo ya maandalizi ya msimu jijini London na imetajwa kusaidia kusukuma maandalizi ya michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2012 katika jiji la London.
miongoni mwa mashabiki waliyojitokeza ni pamoja wachezasoka maarufu nchini Uingereza Jermain Defoe, Joe Cole, Sol Campbell, Darren Bent na Michael Dawson, bingwa wa kuruka chini ama triple jumper Phillips Idowu, Bondia David Haye, Nyota wa mchezo wa rugby Joe Worsley na Steve Borthwick na boy band JLS.

Tuesday, October 6, 2009

SERENA WILLIAMS SASA NAMBARI MOJA DUNIANI KATIKA TENIS

Serena Williams amefanikiwa kuinyakua nafasi ya kwanza katika viwango vya Tenis Duniani baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Ekaterina Makarova katika hatua ya pili ya michuano ya wazi ya China ambayo inafanyika Beijing.
Williams mwenye umri wa miaka 28, alimchapa Mrusi huyo kwa seti 6-3 6-2 na kuchukua nafasi hiyo ya juu kwasababu amefanikiwa kusonga mbele zaidi kuliko aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza Duniani Dinara Safina.
Mmarekani Williams saa moja lilitosha kumuondosha Makarova mwenye umri wa miaka 21.
Mcheza Tenis wa Urusi, Safina ambaye sasa anaumri wa miaka 23, alipoteza mchezo wake na Mchina Zhang Shuai katika mzunguko wa pili.
Serena Williams amesema amefurahi kupata nafasi hiyo kwasababu amekuwa akifanya juhudi kubwa mwaka huu kufika hapo.
ALiyekuwa akishikilia nambari 15 Duniani Maria Sharapova amefanikiwa kupanda baada ya kujitutumua kwa ushindi na kupanda hadi nafasi ya tatu baada ya kumchapa nambari tisa Duniani Victoria Azarenka kwa seti 6-3 6-7 7-5.

Sunday, October 4, 2009

KATIKA LIGI KUU TANZANIA BARA AZAM NA JKT RUVU SARE


Beki wa timu ya Azam Ibrahim Shikanda (kushoto) akichuana na mchezaji wa JKT Ruvu, Damasi Makwaya wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Timu hizo zilifungana bao 1-1.Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Danny Wagaruka (kushoto) akitafuta njia ya kumpita mlinzi wa JKT Ruvu, Kessy Mapande wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Timu hizo zilifungana bao 1-1.

ROAD TO MAMA AFRIKA YA ZAIN, D BANJ AFANYA KWELI

Jamani jamani kumbe hadi mwanamuziki hufurahia kazi yake jukwaani eeehHawa ni mashabiki wakiruka debe LIVEHuyu mwenye Nyeupe ni D Banj akiwajibika.
AY ni moja ya wasanii wanaowania tuzo ya MTV
AY na hatua za jukwaani
Mwimbaji wa muziki wa kizaza kimpya nchini Abwene Yesai AY akiwajibika wakati wa onesho la Road to mama Tanzania iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Zain Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)Wabongo hawakonyuma na hivi siku hizi simu zina videocamera full kurekodiProffesa Jay naye hakuwa nyuma kuwarussha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, kweli jamaa sasa kawa Daddywatu weeeewe Jay wamitulingaShaa naye hakusita kuwathibitishia mashabiki kwmaba huu ni wakati wake.

SIMBA HAIKAMATIKI LIGI KUU TANZANIA BARA

Simba weeeeeweeeeeeeeeHapa hupati kitu, ndo nakwenda hivyoSimba yazidi kujikita kileleni
Simba 2 - 1 Moro United
Wafungaji
Danny Mrwanda dk 23 Yona Ndabila dk 57
Joseph Owini dk 84

Mtibwa 3 - 1 Tanzania Prison
Saidi Rasgudu Ramadhani Katabalala
Soud Abdallah
Hussein Jabu

Toto African 0 - 0 Majimaji

Kagera Suger 0 - 2 Yanga
Mrisho Ngasa dk 17
Jerison Tegete dk 72

MISS TANZANIA MIRIAM GERALD AKABIDHIA MILIONI KUMI ZAKE

Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom, Bob Collymore (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni.9 kwa mshindi wa mashindano ya urembo wa Vodacom miss Tanzania Mariam Gerald, wakati wa sherehe za kumpongeza mrembo huyo na kugawa zawadi kwa washindi iliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki.(Picha na Rajabu Mhamila)Meneja wa Bia ya Redds Kabula Nshimo(kulia)akimkabidhi Miss Tanzania ambaye aliibuka pia mshindi wa Miss Photogenic Miriam Gerald katika hafla iliyofanyika Giraff Hotel, Dar es Salaam. Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D Mnyamwezi

Saturday, October 3, 2009

NDONDI - CHEKA AMBWAGA KASEBA

BINGWA wa Dunia wa uzito wa middle anayeshikilia taji ya ICB, Francis Cheka jana usiku alifanikiwa kuutetea mkanda wake baada ya kumtwanga bingwa wa Dunia wa Kickboxer, Japhet Kaseba kwa TKO.
Cheka anashikilia mkanda huo tangu mwaka jana baada ya kumtwanga kwa KO Hassan Matumla katika raundi ya 10 ya mchezo wao.
Pambano hilo lililoshihudiwa na mamia ya wapenzi wa mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Kaseba ambaye alionesha ukomavu baada ya kuweza kumihili ngumi nzito za Cheka katika raundi nane zilizopita lakini raundi yatisa alishindwa kuhimili kishindo hicho baada ya kukubali kwenda chini baada ya kutwishwa ngumi nzito lililompereka kwenye kamba na kuanguka chini.
Cheka ambaye alitamba kummaliza Kaseba baada ya raundi ya sita alifanikiwa kufanya hivyo katika raundi hiyo ambapo alimpiga mpinzani wake ngumu ya kidevu na kujikuta akiwa chini.
Baada ya ngumi hiyo mwamuzi wa mchezaji huo, Antony Lutta alisimamisha pambano na kumwesabia na Kaseba alikuwa tayari kuendelea na pambano hilo.
Cheka kwa kuwa alikuwa tayari kwa kummaliza Kaseba alimvamia na kumsukuma kwa ngumi ambayo ilimfanya Kaseba aende tena chini lakini hata mwamuzi aliposimamisha mchezo Cheka hakusikia na kuendelea kumshambulia.Hali ya kushambuliwa Kaseba bila kikomo ilimshinda msaidizi wake na kuamua kuingia ulingoni na kumbeba Cheka na kumtupa nje ya ulingoni.
Baada ya tukio hilo pambano lilivulugwa kutokana na fujo zilizokea pande mbili za mashabiki wa mabondia hayo.
Kutokana na vulugu hizo mwamuzi wa pambano hilo aliamua kumpa ubingwa Cheka kwa kuwa kitendo kilichofanywa na msaidizi wa Kaseba ni sawa na kutupa taulo kumwokoa bondia wake.Kwa kipigo alichopokea Kaseba kinadhihirisha kuwa bondia huyo kutoka mkoani Morogoro kuwa bado hana mpinzani katika ramani ya mchezo huo kwa sasa baada ya kuwachapa ndugu wawili, Hassan na Rashid Matumla.Cheka alianza kutawala mpambano huo tangu raundi ya nne kutokana na kupata nafasi ya kumshambulia mpinzani wake kutokana na mtindo wake wa kuzuia zaidi.
Mpambano huo ulitanguliwa na mapambano ya utangulizi ambapo Mada Maugo alimtwanga wa KO Kanda Kabongo katika raundi ya pili, Habibu Pengo alimchapa kwa KO raundi ya kwanza Adrias Charles na Francis Suba alipigwa kwa pointi na Antony Mwakapalila.
Mapambano mengine ni Lesekelo Daud alimshinda kwa pointi Baraka Nuhu, Charles Mashari alishinda kwa pointi Omary Ramadhani, Habibu Mganda alimchapa kwa pointi Sadick Momba na mchezo pekee wa wasichana kati ya Pendo Njau aliyemtwanga kwa pointi Flora Paul.Katika michezo ya Kickboxing Mrisho Van Damme alimtwanga kwa KO Mrisho Jumanne, Emmanuel Shija alimchapa kwa KO raundi ya pili Mohamed Kidevu na Shukuru Samata alishinda kwa KO raundi ya pili Said Kuchi.
Mpambano huo wa ubingwa kati ya Cheka na Kaseba ulidhaminiwa na kampuni ya Business Times Ltd wachapishaji wa magazeti ya Majira, Business Times, Dar Leo na gazeti la michezo la Spoti Starehe linalokuwa mtaani kila Alhamisi na Jumapili na Zain.
Bondia Mada Maugo wa Tanzania akitupa konde la kushoto kwa mpinzani wake Kand Kabongo wa Zaire wakati wa pambano lao la kirafiki lililofanyika Dar es salaam juzi Maugo alishinda kwa KO ya raundi ya pili.(Picha na Rajabu Mhamila)Dakitari Killaga Kulwa (kushoto) akimpatia huduma ya kwanza bondia Mfaume jumane baada ya kupasuka juu ya jicho wakati wa mchezo wa Kick Boxer uliofanyika Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)Bondia Pendo Njau (kushoto) akimpiga ngumi mpinzani wake Flora Malecela wakati wa pambano lao lililofanyika Dar es salaam juzi Pendo alishinda kwa pointi.(Picha na Rajabu Mhamila)Asikari polisi akiwa amemkamata mmoja wa mashajabiki waliokuwa wanaleta fujo wakati wa pambano la ngumi za kugombania mkanda wa Dunia ICD kati ya Japhet Kaseba na Fransisi Cheka uliofanyika Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)

MIRIAM GERALD MISS TANZANIA 2009

JIJI la Mwanza limeendelea kutesa katika fani ya urembo baada ya juzi usiku mrembo Miriam Gerald kufanikiwa kutwaa taji Miss Tanzania 2009, shindano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Mwanza imewatesa warembo kutoka mikoa ya Tanzania baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa miaka miwili mfufulizo baada ya mwaka jana taji hilo kunyakuliwa na Nasreem Karimu naye kutoka jiji hilo.
Miriam ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, pia jana alifanikiwa kuondoka na Suzuki Vitara mpya.Mbali na taji hilo pia Miriam ndio Mrembo mwenye mwonekano mzuri katika picha baada ya kunyakua taji la Redd's Photogenic na kujinyakulia kitita cha sh. milioni moja na mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi za kinywaji cha Redd's.
Nyota ya Miriam ilianza kung'ara tangu mapema kwani kila alipopanda jukwaani katika mavazi mbali mashabiki walimshangilia kwa kelele kutokana na urembo wake.
Miriam alipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki baada ya kuamua kujibu swali aliloulizwa kwa kiswahili kwa kuwa ndio lugha yake ya Taifa, hali iliyoamsha ndelemo na vifijo ukumbini hapo.Nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo kutoka Ukanda wa Vyuo Vikuu, Beatrice Lukindo wakati mrembo aliyeiwakilisha kanda ya Ilala, Judith William alishika nafasi ya tatu.
Nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo kutoka Silvya Shally kutoka Ilala na nafasi ya tano ilikwenda kwa Sia Ndasoki aliyeiwakilisha kanda ya Temeke.
Warembo 10 kati ya 29 waliofanikiwa kuingia katika hatua ya 10 bora ni Miriam Gerald, Beatrice Lukindo, Julieth William, Silvya Shally, Sia Ndasoki, Ivony Birigwa, Susan Emmanuel, Gladys Shao na Evelyne Gamasa.
Warembo wengine ambao walifanikiwa ktwaa mataji mengine ni Tory Oscar aliyetwaa taji la mrtembo mwenye kipaji na kujinyakulia sh. 500,000 kutoka hoteli ya Giraffe Ocean View.
Mwingine ni Judith William ambaye ametwaa taji la kuwa balozi wa Utalii wa ndani na kujinyakulia zawadi zenye thamani ya sh. milioni 3.3 kutoka kwa Bodi ya Utalii Tanzania.Mrembo huo amejinyakulia compyuta ndogo (laptop) mpya pamoja na pesa taslimu sh. 1,100,000.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo ni Glory Chuwa (Tanga), Jackline Nitwa (Dodoma), Shany Anthony (Temeke), Wagala Shungu (Higher Learning Institute).
Wengine ni Julieth Willium (Ilala), Sabina Bododi (Mara), Stellah Chidodo (Singida Kanda ya Kati), Ester Gao (Higher Learning Institute), Doris Deogratius (Higher Learning Institute), Sandra Malebeka (Kinondoni), Stella Solomoni (Temeke) na Mary Lucas (Southern Hinglands).Pia wapo Aloycia Innocent (Kinondoni), Precious Donald (Pwani), Maria Daniel (Arusha), Gloria Mayowa (Lindi), Lulu Ibrahimu (Kinondoni), Glory Willium (Ilala), Catherine Letara (Southern Hinglands) na Mary Joseph (Mara).
Shindano hilo ambalo lilifurika watu wengi lilipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa asili ikiwa pamoja na muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii maarufu nchini pamoja na Uganda.

RICH RICH AJITOKEZA TENA

Muigizaji Maarufu nchini Single Mtambalike Rich Rich akizungumza na waandishi wa habari waandamizi wa magazeti nchini Saidi Mwishehe mwenye karatasi na Piter Mwenda wa gazeti la MajiraPicha zote na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi

Thursday, October 1, 2009

CHEKA VS KASEBA NANI MBABE ?

Mratibu wa wa mpambano wa ngumi, Ramadhani Uhadi katikati akiwainuwa mikono Dar es salaam jana mabondia, Japhet Kaseba (kushoto)na Francis Cheka kabla ya kupima uzito kwa ajiri ya mpambano wao leo.(Picha na Rajabu Mhamila)BOndia Japhet Kaseba (kushoto) na Francis Cheka wakitunishiana misuri Dar es salaam jana baada ya kupima uzito kwa ajiri ya mpambano wao leo.(PIcha na Rajabu Mhamila)

TBL YAZINDUA CHUPA MPYA YA NDOVU

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL) Bw. Robin Goetzsche (kulia) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw. David Minja (kushoto) pamoja na Meneja wa bia ya ndovu Bw.Oscar Shelukindo wakifuraia baada ya kuzindua chupa mpya ya bia ya Ndovu Special Malt Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)

CCM WACHUKUA FOMU KIWALANI

Msimamizi wa Uchaguzi Msaidizi Mtaa wa Yombo Kata ya Kiwalani, Bw. Ignes Maembe (kushoto) akimkabidhi fomu ya kugombea uwenyekiti wa mtaa wa Yombo,Bw. Athumani Maembe Dar es salaam jana wa pili kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wa kata hiyo Bi.Rahma Mnyachi na Diwani wa kata hiyo Bw.Said Abdallah.(Picha na Rajabu Mhamila)

ZAIN NA BUILD OUR NATION (BON)

Meneja wa huduma kwa Jamii wa Zain Tanzania, Bi.Tunu Kavishe (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusu kutimiza miaki mitano ya Programu yake ya kusaidia jamii Build Our Nation (BON) ambapo wamepanga kusherekea kwa sataili ya pekee kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii Mkoani Tabora na Dar es salaam (kushoto) ni Meneja wa kitengo cha wateja wa Kampuni hiyo Bi.Lene Brown.(PIcha na Rajabu Mhamila)

TASAF NA UHAWILISHAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTAWALA BORA) Bi. Sophia Simba (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi laki tano na elfu arobani kwa mwenyekiti wa kamati wa kijiji cha Msufini Mkoa wa Pwani,Bi.Sauda Ramadhani, wakati wa ufunguzi wa Mpango wa kijamii wa uhawilishaji fedha kwa kaya masikini uliozinduliwa Kibaha mkoa wa Pwani jana anaeshughudia katikati ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) ambao ni wafadhiri wa mradi uho, Drk, Servaciaus Likwelile.(Picha na Rajabu Mhamila)Wasanii wa kikundi cha ngoma za Asili cha Mlandizi Theatre group wakiwajibika wakati wa ufunguzi wa Mpango wa kijamii wa uhawilishaji fedha kwa kaya masikini uliofanyika Kibaha Maili moja jana.(Picha na Rajabu Mhamila)Na Rajabu Mhamila

SERIKALI imewataka wananchi walioingia katika awamu ya kwanza ya mradi wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), kutumia vyema mpango huo, ili uweze kuwa endelevbu katika wilaya na mikoa mingine hapa nchini.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba mjini hapa juzi, wakati akizindua mpango huo katika viwanja vya Mailimoja, ambapo alisema Serikali ya awamu ya nne imedhamiria kuboresha maisha kwa watu wenye kipato cha chini.
Alisema wakati Serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani, Rais Jakaya Kikwete alikutana na wabunge na kuelezea azma ya kuhakikisha inaboresha maisha kwa watu wenye kipato kidogo, kwa lengo la kupunguza umasikini wa kipato.
“Serikali imedhamiria mambo mengi ya kuwafanyia wananchi wake na kuazimia kuweka mikakati imara, itayowezesha kuinua hali ya maisha kwa ustawi wa jamii na kuimarisha utawala bora na katika kufanikisha hilo, imekuwa ikifanya mengi kwa kushirikiana na mashirikia mbalimbali,” ilisema Simba.
Alisema kwa kudhihirisha hilo, TASAF ilianzishwa ambapo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali muhimu kwa jamii kwa lengo la kuhakikisha inapunguza matatizo yanayowakabili wananchi, kama si kumaliza kabisa na kuelezea mpango mpya na kusema kuwa wakati ikiendelea na mchakato huo kwa sasa imekuja na mpango mpya wa Uhawilishaji wa Fedha kwa Kaya Masikini, unaoendeshwa na TASAF.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Dkt. Servacius Likwelile alisema mpango huo ulianza miaka mitatu iliyopita, ambapo walianza kwa kufanya uchunguzi vijijini kufahamu nini matatizo yanayowakabili wananachi na kufanikiwa kukutana na matatizo mbalimbali kabla ya kwenda kuyafanyia kazi.
“Katika vijiji tulivyotembelea tumekutana na matatizo mengi, ambayo kati yao yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya wazazi wa kiume kukimbia fdamilia zao, hali iliyokuwa ikisababisha mtoto kufikia hatua ya kuacha masomo na kuanza kuwa tegemezi katika familia,” alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema matatizo mengine, ambayo yameonekana kuwa kikwazo ni namna ya ushiriki wao katika mpango wa kuboresha huduma za matibabu, ambapo wengi wao wameshindwa kulipia huduma za afya hali iliyowafanya kushindwa kupata huduma za matibabu, pamoja na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kibaha, Bi. Halima Kihemba ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, alisema mpango huo utakuwa mkombozi kwa wananchi hao, hivyo amewaomba kuhakikisha wanautumia kwa malengo yaloyokusudiwa, ili uweze kuendelea.
Katika uzinduzi huo ambao utazinufaisha wilaya za Kibaha, Bagamoyo na Chamwino iliyopo mkoani Dodoma, kijiji cha Msufini kilikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. 540,000 na kijiji cha Kipangege kilipata sh. 877,500 kwa ajili ya kutoa kwa kaya maskini ambazo zitaanza kufaidika na mpango huo.