Mwanza imewatesa warembo kutoka mikoa ya Tanzania baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa miaka miwili mfufulizo baada ya mwaka jana taji hilo kunyakuliwa na Nasreem Karimu naye kutoka jiji hilo.
Miriam ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, pia jana alifanikiwa kuondoka na Suzuki Vitara mpya.
Nyota ya Miriam ilianza kung'ara tangu mapema kwani kila alipopanda jukwaani katika mavazi mbali mashabiki walimshangilia kwa kelele kutokana na urembo wake.
Miriam alipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki baada ya kuamua kujibu swali aliloulizwa kwa kiswahili kwa kuwa ndio lugha yake ya Taifa, hali iliyoamsha ndelemo na vifijo ukumbini hapo.
Nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo kutoka Silvya Shally kutoka Ilala na nafasi ya tano ilikwenda kwa Sia Ndasoki aliyeiwakilisha kanda ya Temeke.
Warembo 10 kati ya 29 waliofanikiwa kuingia katika hatua ya 10 bora ni Miriam Gerald, Beatrice Lukindo, Julieth William, Silvya Shally, Sia Ndasoki, Ivony Birigwa, Susan Emmanuel, Gladys Shao na Evelyne Gamasa.
Warembo wengine ambao walifanikiwa ktwaa mataji mengine ni Tory Oscar aliyetwaa taji la mrtembo mwenye kipaji na kujinyakulia sh. 500,000 kutoka hoteli ya Giraffe Ocean View.
Mwingine ni Judith William ambaye ametwaa taji la kuwa balozi wa Utalii wa ndani na kujinyakulia zawadi zenye thamani ya sh. milioni 3.3 kutoka kwa Bodi ya Utalii Tanzania.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo ni Glory Chuwa (Tanga), Jackline Nitwa (Dodoma), Shany Anthony (Temeke), Wagala Shungu (Higher Learning Institute).
Wengine ni Julieth Willium (Ilala), Sabina Bododi (Mara), Stellah Chidodo (Singida Kanda ya Kati), Ester Gao (Higher Learning Institute), Doris Deogratius (Higher Learning Institute), Sandra Malebeka (Kinondoni), Stella Solomoni (Temeke) na Mary Lucas (Southern Hinglands).
Shindano hilo ambalo lilifurika watu wengi lilipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa asili ikiwa pamoja na muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii maarufu nchini pamoja na Uganda.
Your own pоѕt haѕ established helpful to us.
ReplyDeleteIt’s ехtгemely uѕeful аnԁ yοu're certainly very educated in this field. You have got opened up my own sight to be able to numerous views on this matter with intriguing and solid content.
My weblog viagra