
Katibu mkuu wa chama hicho George Wesonga ameishutumu kamati ya IOlimpiki ya Kenya na kocha wa zamani kwa kutumia vibaya tiketi za wachezaji kwa kuchukua viongozi wengi kuelekea Denmark.
Amebainisha kwamba wamelazimika kuwaacha Mohamud Ali ambaye alitwa medali ya fedha mwaka 2007 katika michuano ya Dunia pamoja na Yahya Mohamed.
Wesonga sasa amemtaka waziri wa michezo wa Kenya Prof. Hellen Sambili kuingilia kati swala hilo na kuwapa nafasi wachezaji zaidi.
Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo huo inatarajiwa kuondoka siku ya Jumanne wiki ijayo ikiwa ni siku moja kabla ya michuano hiyo kuanza.
No comments :
Post a Comment