Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Yanga wameendeleza wimbi la ushindi kwa timu za mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kuichapa leo Toto African ya Mwanza bao 1-0 katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA jijini Mwanza.
Goli pekee la ushindi lilifungwa na mchezaji Mrisho Khalfani Ngasa katika kipindi cha kwanza baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Abdi Kasim.
Kufuatia ushindi huo sasa Yanga inafikisha jumla ya Pointi 14 na kushika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba ambayo inajumla ya pointi 18.
Kwa mujibu wa Msemaji wa klabu ya Yanga Luis Sendeu amesema kikosi cha Yanga kitaondoka kesho Jijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itacheza michezo mitatu ya kirafiki katika uwanja wa Kambarage na uwanja wa Kahama, kisha itatua mkoani Singida kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na Singida United.
Michezo mingine iliyochezwa leo katika ligi kuu Tanzania bara ni pamoja na Kagera Suger ambayo imetoka sare ya bila kufungana na Maji maji katika uwanja wa Kaitaba, Kagera.Wakati Moro United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya JKT Ruvu.
Wafungaji wa Moro United ni Yona Ndabila aliyefunga goli la kwanza dakika ya 10 baada ya kuunganisha mpira wa kona uliyopigwa na Hussein Swedi, na goli la pili lilipatikana katika dakika ya 34 likifungwa na mchezaji Saidi Ahmed.
Goli la kufutia machozi la JKT Ruvu lilifungwa na Hussein Bunu katika dakika ya 45 akiunganisha krosi iliyopigwa na Sostenesi Manyasi.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment