Amry Massare mtangazaji wa kipindi cha Michezo na kipindi cha Viwanjani kinachorushwa siku ya Jumapili (12:00pm - 13:00pm) na mdau nambari moja wa viwanjani.blogspot.com akimuelekeza jambo katibu wa SPUTANZA Abeid Kasabalala mara baada ya mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha viwanjani Radio Times FM.
Wachezaji wa soka nchini Tanzania wametakiwa kujiandikisha na kuwa wanachama katika chama cha wachezaji nchini Tanzania SPUTANZA chombo ambacho kimeundwa kupigania maslahi ya wachezaji.Hayo yamesemwa na katibu msaidizi wa SPUTANZA Abeid Kasabalala wakati akihojiwa katika kipindi cha VIWANJANI kinachorushwa na Radio Times fm Dar es Salaam kila siku ya Jumapili kuanzia saa sita kamili hadi sasa saba.
Kasabalala amesema anawashangaa wachezaji wa Tanzania hulalamika na kuhitaji msaada wakati tayari wakiwa na matatizo au mambo yanapowawia vigumu na wasijue wapi pa kukimbilia.
Amesema chombo hicho ni chao na ili waweze kukitumia wanalazimika kujiunga na kuwa wanachama.Miongoni mwa faida kubwa ambazo wachezaji wanaweza kufaidia na SPUTANZA ni pamoja na mikataba ambayo wanaingia na klabu zao lakini pia kuwasaidia kudai maslahi yao pindi wanapotimuliwa na klabu ama kusitishwa kwa mkataba wa mchezaji.
Amesema kwa sasa wameanza kutoa mafunzo maalumu kwa wachezaji ili kuwaelimisha na kuwafahamisha faida za SPUTANZA lakini pia kuwafundisha sheria mbali mbali za soka pamoja na taratibu za mikataba na wajibu wao kama wachezaji.Katibu wa chama cha wachezaji wa soka nchini Tanzania SPUTANZA Abeid Kasabalala akijibu jambo katika kipindi cha viwanjani Radio Times FM.
WASILIANA NA SPUTANZA (SOCCER PLAYERS UNION OF TANZANIA)
P.o.Box 13162, Dar es Salaam - POSTA HSE. - GHANA/OHIO AVENUE 4th FLOOR ROOM #403
SIMU - +255754270815, EMAIL: soccertanz@yahoo.com
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment