TAKWIMU MUHIMU
Hadi Simba na Yanga zinapambana hapo kesho Takwimu zinaonesha kuwa lango la Timu ya Simba limeguswa mara 3 tu katika mechi walizoshinda.
Waliifunga Toto African 3-1, 2-1 dhidi ya Moro United na 4-1 kwa JKT Ruvu huku Simba ikiwa imefunga mabao 18 hadi sasa.
Kwa upande wa Yanga Nyavu zake zimeguswa mara 7 huku imefunga magoli 13 katika kuchomoza kwao mara 5, Sanjari 3 na kuzabwa mara moja.
Matokeo ya Jumla yanatanabaisha kuwa Yanga na Simba zimekutana mara 82 huku Simba ikishinda mara 30, Yanga mara 24 zilizobaki ni Suluhu.Mchezaji atakayekuwa na mvuto kwa mashabiki wengi ni kipa Juma Kaseja kutokana na Wana Yanga kutarajiwa kuangalia atafanya nini atakavyosimama langoni mwa Simba kumbuka Kaseja alikuwa Jangwani msimu uliopita kabla ya kurejea Msimbazi msimu huu.
Wachezaji wa Simba wanaotakiwa kuchungwa kwa hali ya juu ni Danny Mrwanda , Emmanuel Okwi, Viungo Hillary Echesa na Mussa Hassan ‘Mgosi’ wakali hao wakiwa sanjari na wenzao Kelvin Yondani, Joseph Owino, Nico Nyagawa, Mohamed Banka, Mohamed Kijuso na Ramadhan Redondo wanaweza kupeleka Simanzi Jangwani.
Mnyama atawakosa mchezo huu ni pamoja na Emeh Izechukwu na Henry Joseph waliouzwa katika klabu ya Kongsvinga ya Norway huku pia wakimkosa Haruna Moshi “Boban” aliyekwenda Sweden kwa majaribio ya kucheza soka la kimataifa.
Kwa upande wa Yanga wachezaji wanaotakiwa kulindwa kwa umakini ni Mike Barasa, Jerson Tegete, Mrisho Ngassa, Athuman Iddi’Chuji’ , Kabonge Honore na Nurdin Bakari.
Wachezaji ambao wamewahi kucheza katika klabu ya Simba na Yanga na wanatarajiwa kuteremka Dimbani hapo kesho ni pamoja na Juma Kaseja, Athumani Iddi “chuji’, Nurdin Bakari na George Owino.
Kwa upande wa Yanga watawakosa Nadir Haroub ‘Cannavaro” na Ben Mwalala, Nadir “Canavaro’ anasukuma soka la kulipwa katika klabu ya Vancouver Whitecaps ya CANADA.
Mwamuzi wa Mtanange huo anataraji kuwa Oden Mbaga ambaye katika mchezo uliyopita alikuwa mwamuzi wa mezani hivyo anauzoefu wa presha za mchezo wa Simba na Yanga.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment