Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeandaa mpango wa kukuza na kuendeleza soka kwa vijana wadogo hapa Nchini Tanzania utakaoanza mwezi March Mwakani ikiwa ni mikakati waliyonayo ya kuhakikisha mchezo huo unaendelea kukua Duniani kote.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Mjumbe kutoka Fifa Ashford Mamelod amesema mpango huo utaanza Mashuleni kwa kuanza na vijana wakike na wakiume wa umri mdogo ambao ni muafaka kwa kuanza kufundishwa mpira.
Ashford ameongeza kuwa anahitaji ushirikiano mkubwa hasa kutoka TFF na Serikali na Wadhamini katika kuhakikisha mpango huu unafanikiwa kwa asilimia kubwa ili baadae waje kupata wachezaji wazuri wa Kimataifa.
Kwa upande wake Raisi wa Shirikisho la soka Nchini TFF Leodga Chilla Tenga amesema amefurahishwa na mpango huo ijapokuwa inahitajika nguvu za ziada katika kusimamia ikiwa ni pamoja na ushirikiano.
No comments :
Post a Comment