Uongozi wa klabu ya Yanga unataraji kuwasilisha barua katika Shirikisho la Kandanda TFF, Kupinga maamuzi yaliyotolewa na kamati ya mashindano kuwafungia waamuzi wanne maisha na kuitaka klabu ya maji maji ya Songea kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi (10) kama faini kabla ya kuanza msimu wa pili wa Ligi kuu kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Mahugira Madega amesema yawezekana hawakuangalia vizuri adhabu waliyoitoa kutokana na kosa lenyewe katika rushwa, kwani mtoaji na mpokeaji wanatakiwa wawe na adhabu sawa.
Ameongeza kuwa Viongozi wa Maji maji ya Songea nao wafungiwe maisha kama waamuzi na Majimaji ishushwe daraja kwa kuwa Sheria iko wazi hata kimataifa ndio maana Juventus ilishushwa daraja baada ya kubainika imefanya udanganyifu.
HATUA HIYO IMEKUJA KUFUATIA TAARIFA HII ILIYOTOLEWA JANA NA TFF
Kamati ya mashindano ya Shirikisho la soka Nchini Tff limewafungia Waamuzi wanne maisha, pia na kuitaka klabu ya Maji maji ya Songea kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi 10 kama faini kabla ya kuanza msimu wa pili wa Ligi kuu kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Tff Afisa habari wa Shirikisho hilo Frolian Kaijage amesema kamati hiyo ilikaa jana na kujadili masuala mbalimbali ya Ligi kuu ya Tanzania bara hususani katika mchezo namba 20 kati ya Maji maji na Mtibwa Sukari uliochezwa Septemba 9 mwaka huu.
Kaijage ameongeza kuwa katika kamati hiyo walibainisha mambo makuu manne kabla ya kutoa maamuzi hayo.
Miongoni mwa waamuzi waliyofungiwa maisha ni pamoja na Athumani Kazi.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment