Luol Deng amefurahia mafanikio nyumbani kwao kufuatia Chicago Bulls kuitoa Utah Jazz katika michezo ya mwisho ya maandalizi ya ligi kuu ya mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA mchezo uliyochezwa jijini London.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alimaliza mchezo akiwa anaongoza kwa kunyakua jumla ya pointi 18 na kuifanya Chicago Bulls kushinda kwa vikapu 102-101 mbele ya mashabiki 18,689 waliyohudhuria kutazama mchezo huo.
Hata hivyo Chicago inapaswa kumshukuru zaidi James Johnson ambaye alifanya kazi kubwa kuhakikisha inashinda.
Hii ni mara ya tatu mfululizo klabu zinazoshiriki NBA kucheza michezo ya maandalizi ya msimu jijini London na imetajwa kusaidia kusukuma maandalizi ya michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2012 katika jiji la London.
miongoni mwa mashabiki waliyojitokeza ni pamoja wachezasoka maarufu nchini Uingereza Jermain Defoe, Joe Cole, Sol Campbell, Darren Bent na Michael Dawson, bingwa wa kuruka chini ama triple jumper Phillips Idowu, Bondia David Haye, Nyota wa mchezo wa rugby Joe Worsley na Steve Borthwick na boy band JLS.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment