Tanzania imeshuka kwa nafasi tano katika viwangi vya Fifa Dunia katika msimamo uliyotolewa mapema leo.
Tanzania ambayo katika msimamo wa mwezi uliyopita ilikuwa ikishika nafasi ya 94 hivyo imeshuka hadi nafasi ya 99.
Hata hivyo kwa Ukanda wa Afrika Tanzania imeonekana kama imepanda kwa nafasi moja kwani wakati ikishika nafasi ya 94 Duniani Afrika ilikuwa ikishika nafasi ya 23, lakini kwa sasa Afrika inashika nafasi ya 22.
Kuporomoka kwa Tanzania kumetokana na kutoshiriki katika mashindano ya mbali mbali ya kimataifa ambayo hutumiwa na shirikisho la kandanda Dunia kupandisha nchi ama kushuka katika viwango vya kandanda.
Mataifa yamepanda katika viwango vya kandanda Duniani kutokana na kucheza michezo mingi ya kusaka nafasi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.
Ukanda wa Afrika mwezi uliyopita Ivory Cost ilikuwa juu lakini sasa licha ya kupanda kwa nafasi ya moja lakini imeshuka hadi nafasi ya pili na nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Cameroon ambayo imepanda kwa nafasi 15.
Wakati nambari moja Duniani inaendelea kushikiliwa na Brazili ikifuatiwa na Hispania.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment