ZAWADI za mshindi wa Bongo Star Search mwaka 2009 zimetangazwa leo ambapo mshindi wa kwanza atalipwa kiasi cha shilingi milioni 25, wa pili shilingi milioni 5 wa tatu milioni tatu na nusu, wa nne milion moja na nusu nwa tano milioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa shindano hilo Madam Ritha Paulsen amesema, fainali za mpambano huo zitafanyika usiku wa mkesha wa kumbukumbu ya siku naliyokfa baba wa Taifa mwl Julius Kambarage Nyerere katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Madam Ritha amewataka wapenzi wa BSS kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kushuhdia nani anakuwa mshindi na kujinyakulia pesa hizo ambazo zinaweza kuyakomboa maisha yake kama atakuwa na malengo mazuri.
Mpambano huo wa kumsaka mshindi wa Bss mwaka 2009 ulianza na wasanii 15,000 kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo mpaka sasa katika fainali wamebakia Pascal Casian kutoka Mwanza, Peter msechu wa Kigoma, Jackson George wa Tanga pamoja na Kelvin Mbati anayewakilisha Jiji la Dar es Salaam.
Story writen by Adam Hussein.
mshindi wa kwanza milioni 25 wa pili milioni 5, is it fair jamani???!!
ReplyDelete