Shirikisho la soka nchini TFF limewahakikishia Watanzania katika mchezo wa kesho wa watani wa jadi wa Simba na Yanga kuwa utakuwa na Ulinzi na Usalama kwa muda wote kabla na baada ya mchezo huo .
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela amesema utaratibu mzima umeshakamilika ikiwa ni pamoja na kuwa na Askari wa kutosha watakaokuwepo Uwanja mzima kwa ajili ya kuangalia usalama na shughuli zingine.
Mwakalebela ameongeza kuwa siku ya kesho hakutakuwa na uegeshaji wa magari ndani ya Uwanja huo hivyo wanatakiwa kuegesha magari hayo katika uwanja wa Uhuru na katika viwanja vya nje vya Balaza la Michezo la Taifa BMT.
Wakati huo huo Mwakalebela amesema katika kuhakikisha soka la Tanzania linakuwa wao kama Shirikisho wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongea stesheni ya Super Sports kwa ajili ya kuonyesha mpira huo kwa kuurekodi ili uweze kuonyesha na Stesheni zingine za Afrika.
Mwakalebela amesema siku ya leo wamekutana na Timu zote mbili pamoja na Waamuzi na Makamisaa mapema na kuzungumzia kuhus mchezo wa kesho ili kuwapa nafasi Timu hizo kupata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo mgumu iliojaa ushindani.
Wakati huo huo JESHI la polisi la mkoa wa Dar es Salaam, limejipanga kuweka kamera ili kubaini waanzilishi wa vurugu katika mpambano wa mpira wa miguu kati ya watani wa jadi Simba na Yanga.
Akizungumza Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema, sambamba na kamera hizo pia kutakuwa na namba ya simu ambayo itawaruhusu mashabiki watakao kuwa uwanjani hapo kutuma ujumbe mfupi ili kuwavumbua wahalifu hao.
Kamanda Kova amezitaja namba hizo kuwa ni 0783 034224 ambapo ujumbe utakaotumwa utakuwa ukipita katika kompyuta maalum ambapo utafanyiwa kazi wakati huohuo na maaskari watakao kuwa maeneo hayo.
Amesema, ulinzi umeongezwa mara mbili ili kudhibiti hali yeyote ya utovu wa nidhamu kujitokeza na atakaebainika kufanya uhalifu tachukuliwa hatua hapo hapo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Amesema, hakutaruhusiwa kila mtu kufanya biashara isipo kuwa kutakuwa na watu maalum kwa ajili ya kufanya biashara ili kuepusha purukushani zisizo za lazima ambazo ndizo chanzo cha vurugu.
Hata hivyo, kamanda kova ametahadharisha mashabiki wa Simba kutokuja na jeneza uwanjani kwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na ni kitendo kinachochochea vurugu kwa timu hizo hasa ipatapo ushindi.
Vile vile Kamnda Kova amesema, hakutaruhusiwa uuzwaji wa kilevi cha aina yeyote uwanjani ikiwa ni pamoja na watu kuzingatia gharama za tiketi walizo kata ambapo kila mtu anastahili kukaa sehemu husika.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment