Wenyeji na mabingwa watetezi Nigeria wamemaliza mchezo wao na mabingwa wa Ulaya Ujeruamni kwa kutoka sare ya goli 3-3 katika mchezo wa ufunguzi wa fainali za Dunia chini ya Umri wa miaka 17.
Ujerumani iliwachukua dakika 22 kupata goli kupitia kwa mchezaji Lennart Thy na kuwanyamazisha mashabiki wa Nigeria.
Kama haitoshi dakika 16 baadaye waliongeza goli la pili kupitia kwa mchezaji Shkodran Mustafi.
Timu zote zilirejea uwanjani kwa kasi, lakini ilikuwa ni Ujerumani ambayo ilipata nafasi tena ya kufunga goli la tatu kupitia kwa mchezaji Mario Goetze na kufanya matokeo kuwa 3-0 katika dakika ya 47.
Mpira ulianza kugeuka kwa mabingwa watetezi kunako dakika ya 53 wakati Robert Labus alipompenyezea mpira Omoh Ojabu katika eneo la penati, na kupata penati na kupata goli la kwanza, kupitia kwa mchezaji Stanley Okoro katika dakika 54 wakati mchezaji Kenneth Omeruo akifunga goli la pili dakika tano baadaye.
Mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Edafe Egbedi alifunga goli la tatu katika dakika ya 61 na kuwalazimu kugawana popinti.
Argentina sasa inaongoza kundi A baada ya kuichapa Honduras 1-0.
na katika kundi B Switzerland iliichapa Mexico 2-0.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment