Na Rajabu Mhamila
BENKI ya NMB imejitosa kudhamini mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) yanayotarajia kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, Meneja Mikopo Midogomidogo wa benki hiyo,Mashaga Changarawe amesema wameamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuombwa na viongozi wa shirikisho hilo ambapo kwa kuzingatia kuwa na wao ni wanamichezo na muda mrefu ndio maana wakaamua kudhamini.
Amesema kutokana na wao kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini hawakuwa na budi kuwafadhili wenzao kwa namna moja ama nyingine ambapo wametoa fulana 114 zitakazotumika katika mashindano hayo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Sadiq Sangawe amesema wamefurahi kupata hizo fulana, hivyo watazitumia kama inavyotakikana ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Novemba 6 mpaka Novemba 17, mwaka huu
mgeni rasmi katika ufunguzi huo atakuwa mkuu wa Mkoa wa Tanga, Saidi Kalembo.
No comments :
Post a Comment