Masanja alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili ambapo baadae alifariki Dunia Bw. Gasper amesema habari zaidi zitatolewa baadae lakini Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo imeunda kamati ili kushughulikia masuala yote kuhusiana na msiba huo.
Selestin Masanja alizaliwa Urambo Mkoani Tabora Januari 20 mwaka 1957 na kusoma katia elimu ya msingi hapo baadae alijiunga na shule ya Sekonsari ya Itagana 1972-1975 baadae shule ya Sekondari Minaki 1975-1977.
Mwaka 1988 alienda nchini Cuba katika jiji la Havana na kuchukua shahada ya Uzamili wa Physical Education.
Akiwa mfanyakazi wa Serikali katika idara yaMichezo Marehemu Massanja aliwahi kuwa Afisa michezo mkuu daraja la I, Meneja wa uwanja wa Taifa, Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya TFF, Katibu mkuu wa FAT Msaidizi, Afisa michezo idara ya Michezo, Katibu mkuu msaidizi wa FAT tena Kocha Mkuu wa African Sport ya Tanga
No comments :
Post a Comment