
Kikosi hicho kitashuka uwanjani bila ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa anayecheza soka la kulipwa nchini Ufarnsa katika klabu ya Auxxere Dennis Oliech na Macdonald Mariga.
wakati huo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Tunisia Lassad Nouioui amesema Carthage Eagles wamefanya maandalizi mazuri na wanaamini wataibuka na ushindi.
Kwingineko, kikosi cha Super Eagles cha Nigeria kimerejea mjini Abuja katika uwanja wa taifa kucheza na Msumbiji ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kushindwa kuwafunga vinara wa kundi la 2 Tunisia katika uwanja huo.
Uwanja wa Abuja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 umetajwa pengine usiweze kujaa, kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Kenya na Tunisia.
Msumbiji wanarekodi ya kupoteza michezo miwli mfulululizo dhidi ya Tunisia na Kenya wakicheza ugenini.
Mchezo wa mwisho kushinda ni baada kuichapa Kenya 2-1 huku mfungaji akiwa Tico Tico walipocheza Maputo mwezi uliyopita na kupanda hadi nafasi ya tatu wakkiwa mbele dhidi ya wapinzani wao Kenya.
No comments :
Post a Comment