Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen (kulia)akimkabidhi hundi ya shilingi milion 25 kwa mshindi wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS), Paschal Cassan wakati wa hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika Dar es salaam jana anaeshudia katikati ni Ofisa mwandamizi Mkuu kutoka Balaza la sanaa la Taifa (BASATA) na mlatibu wa BSS, Victoria Temu.(Picha na Rajabu Mhamila)
Na Rajabu Mhamila
KAMPUNI ya Bench Mark Productio , imewakabidhi zawadi zao washindi wa mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji vya Bongo Star Seach BSS 2009.
Zawadi hizo za pesa taslim zilikuwa ni sh. milioni milioni 35.5 zilitolewa kwa washindi watano wa mashindano hayo yaliyomalizika 0ktoba 13 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Washindi waliokabidhiwa zawadi hizo ni nyota wa mashindano hayo ya BSS kwa mwaka 2009 Pascal Cassian aliyekabidhiwa sh. milioni 25, Peter Msechu aliyekabidhiwa sh. milioni tano, Kelvin Mbati aliyepata sh. milioni tatu, Jakson George aliyepata sh. milioni 1.5 na Beatrice William aliyepata sh.milioni moja.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo nyota wa mashindano hayo Cassian amesema kwa kuwa kwake ni mara ya kwanza kushika pesa nyingi kama hizo, atajadiliana na wazazi wake kabla ya yeye kuchukua maamuzi yoyote juu ya kuzitumia pesa hizo.
Mshindi wa tatu wa BSS Kevin Mbati akikabidhiwa milion 3
"Naweza kusema hii ni mara yangu ya kwanza kushika pesa nyingi kama hizi, hivyo kwa kuwa nina wakubwa zangu kama wazazi nitasikiliza kwanza ushauri wao kabla ya kuzitumia,"alisema Cassian.
Amesema kwa sasa anajipanga kutoa nyimbo zake yeye mwenyewe na kwamba yupo katika maandalizi ya mwisho ili kuzikamilisha nyimbo hizo na kuzirusha hewani.
Jackson George mshindi wa nne wa BSS akikabidhiwa kiasi cha Tsh milion 1.5
Naye Mkurugenzi wa Bench Mark Production ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, Ritta Poulsen amesema Bench Mark ipo katika maandalizi ya awali ya kuandaa mashindano ya BSS 2010.
"Tunawaomba vijana ambao wapo na vipaji vya uimbaji wakae tayari kwani tunatarajia kuanza mchakato wa kusaka vipaji hivi mapema ili kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania tunavisaka vipaji hivyo,"amesema Ritta.
Beatrice William mshindi wa tano wa BSS akikabidhiwa fedha taslim Tsh Milioni moja.
Amesema mchakato wa kusaka vipaji hivyo hautakuwa tofauti na miaka iliyopita na kwamba Bench Mark itaboresha zaidi mashindano hayo mwaka hadi mwaka.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment