Majuto Omari akipokea jezi toka kwa meneja udhamini wa Vodacom Emilian Rwejuna
Na Rajabu Mhamila Super d Mnyamwezi
TIMU ya Mpira wa miguu na Netiboli ya bendi ya muziki wa dansi ya African Star 'Twanga Pepeta' kesho itachuana na timu ya waandishi wa habari za michezo (TASWA FC) katika viwanja vya leaders, Dar es Salaam.
Mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi na kumbukumbu za hayati Mwalimu Julius Nyerere ambazo hufanyika Oktoba 14 ya kila mwaka tangu aage Dunia.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa African Star Entertainment (ASET), Asha Baraka alisema, Twanga pepeta wao wapo tayari kwa kucheza na timu hiyo ambapo timu yake imejiandaa kwa ajili ya shamra shamra hizo.
Alisema, sambamba na timu za pande hizo mbili pia wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchini watashiriki kwa pamoja katika kuadhimisha siku hiyo.
Asha alisema, baada ya bonanza hilo, wataelekea katika makazi ya Mwl. Nyerere, Msasani kwa ajili ya kufanya usafi katika makazi hayo ikiwa ni pamoja na kupanda maua katika maeneo ya makazi hayo.
Alisema,wanamuziki na wasanii wengine ikiwa pamoja na waandishi watajifunza mambo mbalimbali aliyokuwa akiyafanya Mwl. Nyerere enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kufahamu makazi yake.
" Nadhani hii ni njia pekee ya kuwafanya vijana hawa kufahamu historia fupi ya Mwalimu ikiwa ni pamoja kufahamu mambo mbalimbali aliyokuwa akiyakemea na kuyapinga kama Rushwa, Udini na Ukabila ili kuepuka machafuko", alisema Asha.
Asha alisema kumbukumbu hizo zitamaliziwa na burudani ya uhakika kutoka kwa bendi hiyo linalofanyika kila siku ya jumatano katika ukumbi wa Klab Billcanas, Posta, Dar es Salaam.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment