Mkenya Samuel Wanjiru, ambaye alishinda katika michezo ya Olimpiki ya Beijing katika marathon mwaka jana, anatarajiwa kukutana na mpinzani mkubwa katika michuano ya Marathon itakayofanyika Chicago Jumapili hii.
Wanjiru, ambaye mwezi ujao anatimiza miaka 23, amepania kuvunja rekodi ya Dunia ya mwanariadha wa Ethiopia Haile Gebrselassie ya kukimbia saa mbili, dakika tatu na sekunde 59 mwaka jana jijini Berlin.
Lakini pia atakuwa amevunja rekodi yake ya muda mzuri wa saa 2:05.10 ambao uliuweka mwezi April jijini London.
Matokeo mazuri aliyapata katika michuano ya majira ya joto mwaka 2008 ambapo alikimbia huku hali ya hewa ikiwa ni ya joto la juu na kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika Olimpiki kwa kukimbia kwa saa 2:06.32, akiwa chini ya rekodi ya Dunia kwa dakika tatu.
Katika michuano minne aliyoshiriki ameshinda mara tatu na kushika nafasi ya pili.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Wanjiru kuzuru nchini Marekani huku akitaraji kuchuana na wanariadha bora kumi toka Afrika, ikijumuisha wanariadha saba toka nchini Kenya, wa Morocco wawili na mmoja toka Ethiopia.
kwa upande wa Wanaume itajumuisha Abderrahim Goumri wa Morocco na Vincent Kipruto wa Kenya.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment