TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
1. RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA CHARLES CELESTIN MASANJA
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limepokea kwa mshtuko mkubwa msiba wa Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Charles Celestin Masanja uliotokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba 19, 2009 nyumbani kwake Kimara Dar es Salaam.
Kwa TFF jamii ya mpira imempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa na ushirikiano mkubwa katika harakati za kusukuma mbele maendeleo ya soka la Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa kifo hiki kimekuja ghafla na katika wakati ambao mchango wake ulikuwa bado unahitajika mno.
Kutokana na ushirikiano wake na watu mablimbali aliofanya nao kazi, Masanja amekuwa ni rafiki wa watu wengi na kwa hakika alikuwa mtu wa watu.
TFF inamtambua Masanja kama mtu aliyekuwa muhimu hasa kutokana na kutumikia vema nyadhifa mbalimbali alizowahi kuzipata katika mpira kama ifuatavyo:
1990 Kocha Mkuu wa klabu ya African Sports ya Tanga.
1993 - 1996 - Katibu Msaidizi wa FAT akiwa ameazimwa kutoka Wizarani
2002 – 2004 - Katibu Mkuu msaidizi wa FAT (wa kucaguliwa)
2005 – 2009 Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya TFF
2007 – 2009 Mkufunzi wa ukocha – Mkoa wa kimashindano wa Temeke
2004 – 2009 Mjumbe wa mkutano Mkuu wa TFF kupitia Chama cha Makocha
(TAFCA)
Mbali na nyadhifa hizo, Charles Masanja alikuwa mmoja wa makocha wa kiwango cha Juu hapa nchini kulingana na vigezo vya TAFCA.
TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu na inawatakia wanafamilia uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Mungu aiweke roho ya Marehemu Charles Celestin Masanja mahali pema peponi, Amen.
Florian Kaijage
AFISA HABARI
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment