
Williams mwenye umri wa miaka 28, alimchapa Mrusi huyo kwa seti 6-3 6-2 na kuchukua nafasi hiyo ya juu kwasababu amefanikiwa kusonga mbele zaidi kuliko aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza Duniani Dinara Safina.
Mmarekani Williams saa moja lilitosha kumuondosha Makarova mwenye umri wa miaka 21.
Mcheza Tenis wa Urusi, Safina ambaye sasa anaumri wa miaka 23, alipoteza mchezo wake na Mchina Zhang Shuai katika mzunguko wa pili.
Serena Williams amesema amefurahi kupata nafasi hiyo kwasababu amekuwa akifanya juhudi kubwa mwaka huu kufika hapo.
ALiyekuwa akishikilia nambari 15 Duniani Maria Sharapova amefanikiwa kupanda baada ya kujitutumua kwa ushindi na kupanda hadi nafasi ya tatu baada ya kumchapa nambari tisa Duniani Victoria Azarenka kwa seti 6-3 6-7 7-5.
No comments :
Post a Comment