katibu mkuu wa wekundu wa msimbazi Mwina Seif Kaduguda akiteta jambo na waandishi wa habari.
Na Rajabu Mhamila
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom inataka mchezo wa watani wa jadi nchini Simba na Yanga uliopangwa kufanyika Oktoba 31 ufanyike katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mchezo huo umepangwa kufanyika katika uwanja Uhuru, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Emilian Rwejuna alisema mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Taifa ambapo utatoa fulsa kwa washindi wa shindano la M-Pesa watashuhudia mchezo katika uwanja huo.
"Tumeandaa shindano kwa mashabiki wa klabu hizo kongwe kuwa watakaposhinda watapata nafasi ya kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa Taifa kutokana na ukubwa wa mchezo huo," alisema Rwejuna.Kushoto ni katibu mkuu wa kuajiriwa wa klabu ya Yanga Laurence Mwalusako.
Alisema wamependekeza mchezo huo ufanyike katika uwanja huo kutokana na kutoa fulsa kwa washindi hao ambao baadhi yao inawezekana kuwa hawakupata nafasi ya kuingia katika uwanja huo ambao haujaanza kutumika rasmi.
"Ukiacha wapenzi wa timu hizo wanaoishi jijini Dar es Salaam ambao wanaweza kuwa wamewahi kuuona uwanja huo lakini shindano hilo litajumuisha wapenzi wa timu hizo wa nchi nzima hivyo uwanja huo utakuwa mnoja ya kivutio kwa mashabiki hao," alisema Rwejuna.
Uwanja huo ambao umezinduliwa rasmi hivi karibuni lakini umekuwa ukitumika kwa michezo ya timu ya Taifa pamoja na baadhi ya michuano mikubwa na michezo kati ya miamba hiyo ya soka Tanzania.
Timu hizo zilikutana katika uwanja huo wakati wa michezo yao yote miwili katika msimu uliopita ambapo katika mchezo wa kwanza Yanga ulishinda bao 1-0 na mzunguko wa pili zilitoka sare ya mabao 2-2.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment