Meneja Matukio wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtigwa (kulia) akizungumza na simu Dar es salaam wakati wa kutafuta washindi waliochangia timu za Yanga na Simba kupitia M-PESA ambao watapata tiketi za VIP pamoja na maradhi popote walipo na kuja kuangalia mpambano wa watani wa jadi utakaopigwa jumamosi hii kushoto ni Msimamizi kutoka bodi ya Michezo ya Kubahatisha,Chiku Saleh.(Picha na Rajabu Mhamila)
KAMPUNI ya simu za mkononi Vodacom imeendesha bahati nasibu ya Vodafone M- PESA kwa ajili ya kuwapa fursa wapenzi na mashabiki wa Klabu ya Simba na Yanga kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ya watani wa jadi itakayofanyika Oktoba 31 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Jumla ya washindi 10 walipatikana katika bahati nasibu hiyo ambapo kila mshindi atakabidhiwa tiketi mbili pamoja na jezi mbili ambapo washindi watano ni wa Klabu ya simba huku watano wakiwa ni wa klabu ya Yanga.
Washindi hao kwa upande wa Simba ni mdau wa viwanjani Rajabu Mhamila 'Super D', Adam Chonya, Husein Lingu, Marry Kaduguda na Thabit Kaisari huku washabiki wa Yanga wakiwa ni Issa Kasim, Ramadhan Fulle, Muhidini Omari, Idrisa Mohamed na Mambo Mkediyo.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kuwataja washindi hao Meneja Matukio wa Vodacom Rukia Mtingwa alisema jumla yamashabiki 240 waliweza kuzichangia timu hizo za Simba na Yanga kupitia huduma hiyo ya M-PESA .
Alisema kati ya mashabiki 240 ni mashabiki 52 walifanikiwa kuingia katika bahati nasibu hiyo kwa upande wa Simba huku Yanga ikiwa na mashabiki 57 ambapo kati yao ni mashabiki 10 ndio waliofanikiwa kupata nafasi hiyo ya kushuhudia mechi ya watani wa jadi hao.
Alisema mpango huo wa kuzichangia timu za Simba na Yanga utakuwa ni endelevu na kwamba wapenzi na mashabiki wa timu hizo wanatakiwa kujiunga na huduma hiyo ili kuziwezesha timu hizo kupata fedha zitakazosaidia kuendesha klabu hizo.
Rukia alisema wapenzi na mashabiki wanatakiwa kuzichangia timu hizo kuanzia kiasi cha sh 2,000 ambapo wapenzi wa Yanga watatuma ujumbe huo kwenda namba 200200 huku mashabiki wa Simba wakituma kwenda namba 500500.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment