Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Bi. Tunu Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya kuchagua wanafunzi nane watakaowadhamini katika masomo ya chuo kikuu kulia ni Mkurugenzi wa Udahili na uhifadhi wa Nyaraka kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Bi.Rose Kiishweko.(Picha na Rajabu Mhamila)
Na Rajabu Mhamila
Zain yachagua 8 kwenye udhamini wa Zain Scholars 2009
DAR ES SALAAM, OKTOBA 26, 2009:Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora za mawasiliano hapa nchini ya Zain leo imewatangaza wanafunzi wanane ambao ni washindi wa tuzo ya masomo ya Zain (Zain Scholars Programme) 2009 watakao patiwa udhamini wa masomo yao katika mpango wa Build Our Nation.
Akiongea kuhusu udhamini huo wa wanafunzi wa Zain Sholars bi Tunu Kavishe alisema Wanafunzi hao waliochaguliwa kuingia katika vyuo vikuu vya Tanzania watapatiwa udhamini wa asilimia 100 usio na malipo yoyote pindi watakapomaliza masomo yao ya elimu ya juu.
Bi Kavishe alieleza kwa mwaka 2009 Zain Scholars programme walio chaguliwa ni Dickson Mutegeki, Invokavit Munisi,Tunu Mangara,Elizabeth Ngatunga,Naomi Elibariki,Frank Shega,Sophia Nahodha na Dominicus Kayombo.
Washindi wa udhamini huu wanane wataungana na wengine 31 kutoka vyuo vikuu mbalimbali ambao tayari wameshaorodheshwa kwenye mpango wa masomo wa Zain,na hivyo kufanya idadi ya washindi kufikia 39 hadi hivi sasa.
Mpango huu ambao ni wa kipekee kabisa hapa nchini upo chini ya mradi ulioasisiwa na kampuni ya Zain ujulikanao kama “Tujenge Taifa Letu (Build Our Nation).Mpango huu unaunga mkono sekta ya elimu ya juu na umekua ukitoa vitabu na nyenzo nyingine za elimu kama computer katika mashule mbalimbali nchini Tanzania.
Mpango huu wa Zain Sholars unaojumuisha nafasi za masomo kwa elimu ya juu ambao hutolewa kwa njia ya ruzuku.Washindi wanachaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu(TCU).Akiongelea kuhusu uteuzi huo Bi Rose Kiisheko ambaye ni mkurugenzi wa udaili alisema uteuzi huu unafanyika kwa haki baada ya matangazo kutolewa na wale wanao chaguliwa hutangazwa kwenye vyombo vya habari.Katika mpango huo wa masomo wa Zain Scholars unaodhaminia na Zain pia wanafunzi hawa watapata nafasi ya kufanya kazi Zain katika kipindi cha likizo au mapumziko.Elimu hii ya vitendo inayotolewa na Zain huwapa wanafunzi nafasi ya kuhudhuria elimu ya vitendo inayosaidia kuwajenga katika misingi imara na uzoefu wa kazi pale wanafunzi hawa wanapomaliza elimu yao..
“Mpaka sasa tuna wanafunzi sita walio maliza elimu yao ya chuo na baadhi yao wameajiriwa na Zain na wengine kuajiriwa na makampuni mashuhuri hapa nchini,”alisema Tunu.
Akiongolea kuhusu faidha alizozipata kutokana na mpango huu wa Zain Scholars Noel Mazoya alijivunia akisema uzoefu wa kazi alioupata kutoka Zain umemsaidia sana kwenye kazi na leo hii amepata ajira na Zain.”Nilikua na fursa ya kujifunza kila wakati nikiwa likizo leo hii na mimi naweza kusema nina uzoefu wa kutosha kuajiriwa kampuni yoyote Tanzania.Kwani Zain imeniwezesha kusoma bila kua na deni baada ya kumaliza shule na pia ilinipa uhuru wa kuchagua wapi nifanye kazi na mimi nimeamua kufanya kazi Zain.Niko katika kitengo cha masoko kwa kifupi naweza kusema nalijua soko la Tanzania ijapookua nimemaliza shule juzi,asante kwa Zain.
Zain imewekeza zaidi ya shilingi bilioni moja hapa Tanzania katika mpango huu wa kusaidia jamii kama sehemu ya mkakati wa kampuni wa kuchangia elimu na kuboresha maisha ya jamii.
Zain imedhamiria kuwajibika katika jamii na itaendelea kutoa mchango wake katika kufanikisha mpango wa kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ili kuweza kuwa na mafanikio chanya ya kiuchumi na kijamii katika Tanzania.
Leo hii Zain kwa kushirikiana na Erickson na Taasisi ya Earth tunasaidia vijiji mbalimbali katika eneo la ukanda wa Ziwa Victoria na Mbola katika sekta mbalimbali ili kusaidia kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment