Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTAWALA BORA) Bi. Sophia Simba (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi laki tano na elfu arobani kwa mwenyekiti wa kamati wa kijiji cha Msufini Mkoa wa Pwani,Bi.Sauda Ramadhani, wakati wa ufunguzi wa Mpango wa kijamii wa uhawilishaji fedha kwa kaya masikini uliozinduliwa Kibaha mkoa wa Pwani jana anaeshughudia katikati ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) ambao ni wafadhiri wa mradi uho, Drk, Servaciaus Likwelile.(Picha na Rajabu Mhamila)Wasanii wa kikundi cha ngoma za Asili cha Mlandizi Theatre group wakiwajibika wakati wa ufunguzi wa Mpango wa kijamii wa uhawilishaji fedha kwa kaya masikini uliofanyika Kibaha Maili moja jana.(Picha na Rajabu Mhamila)Na Rajabu Mhamila
SERIKALI imewataka wananchi walioingia katika awamu ya kwanza ya mradi wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), kutumia vyema mpango huo, ili uweze kuwa endelevbu katika wilaya na mikoa mingine hapa nchini.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba mjini hapa juzi, wakati akizindua mpango huo katika viwanja vya Mailimoja, ambapo alisema Serikali ya awamu ya nne imedhamiria kuboresha maisha kwa watu wenye kipato cha chini.
Alisema wakati Serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani, Rais Jakaya Kikwete alikutana na wabunge na kuelezea azma ya kuhakikisha inaboresha maisha kwa watu wenye kipato kidogo, kwa lengo la kupunguza umasikini wa kipato.
“Serikali imedhamiria mambo mengi ya kuwafanyia wananchi wake na kuazimia kuweka mikakati imara, itayowezesha kuinua hali ya maisha kwa ustawi wa jamii na kuimarisha utawala bora na katika kufanikisha hilo, imekuwa ikifanya mengi kwa kushirikiana na mashirikia mbalimbali,” ilisema Simba.
Alisema kwa kudhihirisha hilo, TASAF ilianzishwa ambapo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali muhimu kwa jamii kwa lengo la kuhakikisha inapunguza matatizo yanayowakabili wananchi, kama si kumaliza kabisa na kuelezea mpango mpya na kusema kuwa wakati ikiendelea na mchakato huo kwa sasa imekuja na mpango mpya wa Uhawilishaji wa Fedha kwa Kaya Masikini, unaoendeshwa na TASAF.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Dkt. Servacius Likwelile alisema mpango huo ulianza miaka mitatu iliyopita, ambapo walianza kwa kufanya uchunguzi vijijini kufahamu nini matatizo yanayowakabili wananachi na kufanikiwa kukutana na matatizo mbalimbali kabla ya kwenda kuyafanyia kazi.
“Katika vijiji tulivyotembelea tumekutana na matatizo mengi, ambayo kati yao yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya wazazi wa kiume kukimbia fdamilia zao, hali iliyokuwa ikisababisha mtoto kufikia hatua ya kuacha masomo na kuanza kuwa tegemezi katika familia,” alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema matatizo mengine, ambayo yameonekana kuwa kikwazo ni namna ya ushiriki wao katika mpango wa kuboresha huduma za matibabu, ambapo wengi wao wameshindwa kulipia huduma za afya hali iliyowafanya kushindwa kupata huduma za matibabu, pamoja na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kibaha, Bi. Halima Kihemba ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, alisema mpango huo utakuwa mkombozi kwa wananchi hao, hivyo amewaomba kuhakikisha wanautumia kwa malengo yaloyokusudiwa, ili uweze kuendelea.
Katika uzinduzi huo ambao utazinufaisha wilaya za Kibaha, Bagamoyo na Chamwino iliyopo mkoani Dodoma, kijiji cha Msufini kilikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. 540,000 na kijiji cha Kipangege kilipata sh. 877,500 kwa ajili ya kutoa kwa kaya maskini ambazo zitaanza kufaidika na mpango huo.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
13 hours ago
No comments :
Post a Comment