
Timu ya Taifa ya Netball ya Tanzania imeanza vema michuano ya kimataifa ya Netball katika uwanja wa Taifa kwa kuichapa Lesotho jumla ya magoli 33 - 19

Lesotho hoi, wakimbizwa mbaya uwanja wa Taifa katika mashindano ya kimataifa

KAMA ANASEMA ....ACHAA

KWANINI HIVI TUSIFANYE VIZURI KIMATAIFA ?

HAPA KWELI LAZIMA TUTISHE... ONA KAZI HII

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya Netiboli,(Taifa Queens), ambaye ni nahodha wa timu hiyo Jackline Sikozi (kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Taifa ya Lesotho, Malestephano Matrepe wakati wa ufunguzi wa mashindano ya netiboli ya kimataifa yaliyofunguliwa Dar es salaam jana.9Picha na Rajabu Mhamila)

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya Netiboli,(Taifa Queens), Judith Kaginja (kushoto) akitafuta njia ya kumtoka mchezaji wa timu ya Taifa ya Lesotho, Lumbata Pitro wakati wa ufunguzi wa mashindano ya netiboli ya kimataifa yaliyofunguliwa Dar es salaam jana Tanzania ilishinda kwa 33 kwa 19.(Picha na Rajabu Mhamila)

Mke wa raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasalimi wachezaji wakti wa ufunguzi wa michuano ya Netball ya kimataifa.
No comments :
Post a Comment