HILI NI BENCHI LA UFUNDI LA KLABU YA AFRICAN LYON WA PILI TOKA KULIA NI KOCHA MRENO EDWARD ALMEIDA AKIFUATILIA MCHEZO.
AFRICAN Lyon imezinduka katika mechi ya Ligi Kuu soka Bara baada ya kuilaza Toto African mabao 6-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Huku wakiwa kwenye mvutano na Kocha wao kutoka Ureno, Eduardo Almeida kutoka Ureno kutokana na Lyon kufanya vibaya jana mambo yalibadilika.
Lyon ikiwa na pointi moja baada ya mechi nne jana ilicharuka na huku ikiongozwa na Mremo huyo ambaye baadhi ya vyombo vya habari viliripoti amefukuzwa iliibuka na ushindi mkubwa tangu ligi hiyo ianze msimu huu.
Timu hiyo yenye makazi yake Mbagala iliwanyanyasa watoto wa Yanga, Toto kama ilivyofanya Liverpool kwa Hull City katika Ligi Kuu ya England jana kwa kushinda 6-1.
Bao la African Lyon lilipatikana dakika ya kwanza kwa shuti la mpira wa adhabu uliopigwa na Rashid Gumbo na kumshinda kipa Hussein Katandula.
Dakika ya 29, Robert Sentongo aliifungia Lyon bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Idrisa Abdallah.
Toto ilipata bao la kwanza dakika ya 61, lililofungwa na Maulid Hanim baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Lyon na kuusukumia mpira wavuni.
Hata hivyo, furaha yao ilizimwa dakika moja baadaye kufuatia bao lililofungwa na Yusuph Soka baada ya kuwatoka mabeki wa Toto na bao la nne lilifungwa pia na Soka.
Mbwana Samatta aliipatia Lyon bao la tano na dakika ya 74 na dakika ya 83, Samata alifunga bao la sita.
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, Kocha Mkuu wa Toto African, Mbwana Makatta, alisema tangu aanze kuifundisha timu hiyo, hajawahi kupata kipigo kama hicho.
Makatta alikiri kuzidiwa na African Lyon na kwamba yote hayo yamesababishwa na baadhi ya wachezaji kuwa na matatizo na uongozi na wengine walipata kadi nyekundu.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
1 week ago
No comments :
Post a Comment