Wachezaji gofu kutoka klabu mbalimbali jijini Dar es Salaam Ijumaa wanatarajiwa kuchuana katika mashindano ya kila wiki ya Zain/Lugalo Fiddle kwenye Uwanja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)Lugalo.
Mashindano hayo ya kila wiki, yanatarajiwa kuanza mchana, na baadaye jioni kutatolewa zawadi kwa washindi ikiwa ni pamoja na simu selula zinazotolewa na wadhamini wa mashindano hayo, kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.
Meneja mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania, Beatrice Singano ambaye amesema jijini Dar es Salaam kuwa Zain inaona fahari ya kudhamini mashindano hayo ya kila wiki ya gofu katika klabu ya Lugalo, ili kusaidia kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. “Zain inaona fahari kudhamini mashindano hayo ambayo yanawakutanisha wachezaji gofu wa rika zote kwa ajili ya michezo na burudani , na tunatumaini udhamini wetu utasaidia kuinua kiwango cha mchezo huo nchini ,” alisema Singano.
“Tunaamini udhamini wetu si kwamba utaongeza tu chachu ya ushindani na kujenga afya za wachezaji , lakini pia utasaidia kuendeleza na kuinua michezo ya Tanzania kwa ujumla, haswa mchezo wa gofu".
Nahodha wa klabu ya gofu ya Lugalo, Koplo Priscus Nyoni ameishukulu Zain kwa kudhamini mashindano hayo ya kila wiki, na kubainisha lengo la mashindano hayo ya kila wiki ni kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu kwa kila rika na kila wiki uwanja unakuwa wazi kwa kila mtu.
“Naishukulu kampuni ya zain kwakutambua umuhimu wa mchezo huu wa gofu pia na wakaribisha wachezaji wote wakaribie kwa kuwa mchezo huu ni wa rika zote pia si wamatajiri pekee ni wa watu wote yani watoto wakubwa na wazee wanaweza kucheza mchezo huu karibuni sana”. Alisema Nyoni
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment