Mnyama Simba amezidi kujikita kileleni katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuizamisha Kagera Suger kwa magoli 2-0.
Goli la kwanza la Simba lilifungwa na mchezaji Haruna Moshi "Boban" katika dakika ya 17 na goli la pili lilifungwa Mohammed Kijuso katika dakika ya 77.
Kufuatia ushindi huo Simba sasa inafikisha jumla ya pointi 12, ikifuatiwa na Mtibwa yenye pointi 9, huku ikiwaacha wapinzani wao Yanga waliyo nafasi ya tano kwa tofauti ya pointi 7.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
big up sana wazee poa sana kwa kutupasha habari hasa sisi tulio nje ya nchi. sasa napenda kujua matokeo ya gemu kati ya mtibwa na majimaji lililopigwa juzi nadhani. matokeo yakoje?
ReplyDeletemdau, UK
Tunashukuru Mdau toka UK kwa kufuatilia habari mbali mbali ambazo tunaziweka katika www.viwanjani.blogspot.com Mchezo kati ya Maji Maji na Mtibwa Suger, Maji maji ilishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa, endelea kuwa nasi na usisite kutupatia maoni yako, habari, na picha ili tuweze kukihidhi mahitaji ya wa Tanzania wengi waliyo nje ya nchi
ReplyDelete