Vipimo kwa bingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 raia wa Afrika Kusini Caster Semenya hadi sasa bado vinautata lakini baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuwa anajinsia mbili ya uke na ume.
Semenya, mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliombwa kufanyiwa vipimo ili kubaini jinsia yake kufuatia kuwashangaza watu katika michuano ya Dunia ya riadha mwaka huu na masaa machache kabla ya kushinda huko Berlin.
Magazeti ya Australia yamedai kwamba Semenya ni mtu mwenye jinsia moja lakini anahisia za jinsia nyingine ama ana jinsia zote mbili kitaalamu wanaita hermaphrodite.
Waziri wa Michezo Makhenkesi Stofile amesisitiza mapema leo kwamba "Caster is a woman, she remains our heroine. We must protect her."
Naye Raisi wa Riadha wa Afrika Kusini Leonard Chuene ameliambia gazeti la Star: kwamba IAAF wamewaambia matokeo ya vipimo yanatatanisha hivyo hawawezi kuwapataia.
Mwenyekiti wa Baraza la taifa la michezo, Butana Komphela ameongeza kuwa "Someone is guilty of leaking her confidential medical information to Australian newspapers."
IAAF imethibitisha kuwa kwa sasa haitatoa kauli yeyote kuhusu Semenya hadi wakati mkutano wa kamati ya utendaji ya IAAF itakapokutana Monaco Novemba 20-21.
Semenya alitwaa uchampion wa Dunia wa mita 800 mjini Berlin mwezi August kwa kuweka rekodi ya kukimbia dakika 55.45, akiwa mbele kwa dakika 2.5 dhidi ya bingwa wa mwaka 2007 Mkenya Janeth Jepkosgei.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment