Jaji mkuu Agostino Ramadhani (kushoto) ambaye ni mlezi wa mpira wa kikapu Tanzania BFT akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la kuchangisha fedha zitakazojenga viwanja sita vya mchezo huo nchini.
Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania Limeandaa tamasha la kihistoria litakalojulikana kama BASKETBALL CHARITY DAY litakaloanza tarehe 17 oktoba,2009 na kuhitimishwa tarehe 24 Oktoba,2009, likiwa na madhumuni ya kuchangia maendeleo ya mpira wa Kikapu Nchini.
Amesema wanatazamia kuwa Mgeni wa heshima ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa jamuhur ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mlezi wa Shirikisho wa shirikisho, atakuwa mgeni rasmi na atajumuika katika kilele cha tamasha hilo.
Katika kufanikisha hilo, siku ya kilele kutakuwa na kadi maalum za aina nne, kadi za dhahabu, ya fedha, ya shaba na za kuchangisha kwa makundi.
Kiwango cha chini cha kuchangia kadi ya dhahabu ni Tsh 500,000/= ambapo kwa kadi ya fedha ni Tsh 300,000 kwa wale watakaochangia chini ya Tsh 300,000/= watapewa kadi ya shaba .
Wale wa kadi ya dhahabu watapata fursa ya kucheza au kushangilia timu ya wachezaji wa zamani.
wale wa kadi ya fedha watakuwa upande wa timu itakayoshindana na timu ya wakongwe.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
1 week ago
No comments :
Post a Comment