Watanzania Ali Kiba, Pretty Poet( Jacqueline Kweka Kibacha) na kampuni ya Bongo UK ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kuwania Tuzo za BEFFTA (Black Entertainment,Film,Fashion,Television and Arts Awards) zinazotarajiwa kufanyikia jijini London tarehe 17 October mwaka huu ndani ya London Hilton Metropole.
Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best International Act huku Pretty Poet akichaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Spoken Word Artist/Poets. Kampuni ya Bongo UK imechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Event Promoters.
Kama ilivyo kawaida ya tuzo siku hizi,kura zinapigwa na wananchi.Wakati ukiwadia kwa zoezi hilo, VIWAJANI itakujulisha.Kwa sasa tunapenda tu kuwapongeza Ali Kiba,Pretty Poet na Bongo UK for the nomination.
Ally Kiba anachuana na Beyonce, Akon na 2face Idibia kuwania tuzo ya Best International Act.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment