Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani cha Radio Times FM Katibu Mkuu wa Shirikisho la kandanda hapa nchini TFF, Fredrick Mwakalebela amesema katika mchezo wa Ligi kuu ya VodaCom Agost 23 mwaka huu uliyochezwa kati ya Yanga na Afrikan Lyon baada ya mchezo mchezaji huyo alitokea sehemu ya wachezaji wa akiba na kumshambulia mwamuzi.
Katika mchezo huo mwamuzi wa kati alikuwa Oden Mbaga, mwamuzi msaidizi namba moja Hamisi Chagwalu na namba mbili Zahara Mohamed.
Wakati huo naye kocha wa klabu hiyo Dusan Condic amefungiwa kutojitokeza katika benchi la Yanga kwa michezo mitatu kufuatia kumtolea mwamuzi msaidizi lugha chafu.
No comments :
Post a Comment