Zambia imealikwa katika michuano ya kombe la Cecafa ambalo linatarajiwa kufanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 28 .
Kenya itaanda mashindano hayo mwaka huu kwa mara ya kwanza katika miaka 17 maofisa wa CECAFA wamesema hii leo.
katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema kuwa nchi zingine mbili kutoka kusini mwa Afrika zimeomba kushiriki michuano hiyo.
lakini Zimbabwe na Malawi wameambiwa kuwa kuna nafasi kwa Taifa moja tu kutoka kusini na kati mwa Afrika.
wazambia wamekuwa wakialikwa katika michuano ya CECAFA tangu mwaka 2007 walipolitwaa kombe hilo huko Ethiopia.
zambia wataungana na wenyeji Kenya,Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan na Somalia, nchi nyingine shiriki ni Rwanda, Burundi, Eritrea, Djibouti na Zanzibar.
makundi mawili ya michuano hiyo yatakua mji mkuu wa Nairobi huku kundi la tatu litakua Mumias karibu na mpaka wa Kenya-Uganda.
jumla ya michezo 26 inatarajiwa kuchezwa katika wiki mbili za michuano ya CECAFA itakayofanyika huko Kenya.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment