
Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (watatu mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tabora Yatima Centre na wafanyakazi wa Zain Tanzania baada ya Mwinyi kufuturu pamoja na watoto na kuwakabidhi msaada wa vyakula uliotolewa na Zain. Futari hiyo iliandaliwa na Zain ilifanyika mjini Tabora Jumatatu jioni ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Zain kusaidia yatima katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
No comments :
Post a Comment