Katibu mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Lucas Antony Kisasa amemkabidhi Nyaraka mbalimbali Katibu Mkuu wa kuajiriwa Laurence Mwalusako, makabidhiano yaliyofanyika katika maskani ya klabu ya Jagwani jijini Dar es Salaam.
Akimkabidhi Nyaraka Lucas Kisasa amewashukuru wanachama na wadau wa klabu hiyo kwa ushirikiano wao waliompa kwa muda wake wote wa Uongozi na amehadi kushirikiana nao kwa kila jambo.
Kisasa amesema mrithi wa nafasi yake anamfahamu vizuri hivyo anamkabidhi nafasi hiyo kwa moyo mkunjufu na ana amini atafanya vizuri.
No comments :
Post a Comment