Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Mh.George Huruma Mkuchika akizungumza na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys baada ya kuwasili nchini.
Waziri wa habari utamaduni na michezo Mh.George Huruma Mkuchika amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys kuwekeza fedha za zawadi walizopatiwa na TFF katika elimu kwa faida na maslahi ya taifa katika soka la kulipwa.
Mkuu wa msafara wa vijana hao Msafiri Mgoi ambaye ni mjumbe wa TFF amesema michuano hiyo ilikuwa imejaa vijeba jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua na CECAFA.
Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imerejea nchini huku ikirejea na ubingwa wa nafasi ya tatu iliyoutwaa katika michuano ya kombe la Chalenji.
Tanzania tuna wajibu wa kuwaenzi vijana wetu kama hawa.. naamini tutatisha miaka ijayo.. ni mambo machache tu TFF ikiyafanyia kazi tutafanya vizuri katika michezo Bongo.. Ebwana Maximo tunakufagilia ile mbaya kwenye kipindi chako.. kaza buti mzazi.. Blog la ukweli hili .. tupe mambo motomoto
ReplyDelete