Akizungumza na kipindi hiki Afisa Habari wa TFF Frolian Loimamu Kaijage amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwapiga msasa kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwa sambamba na kufahamu majukumu yao ya kazi.
Kaijage ameongeza kuwa semina hiyo itaongozwa na Mkufunzi ambae pia ni Mjumbe wa Fifa Henry Tandau.
Wakati huo huo, Kaijage amewataka wadau na wapenzi wa mpira wa miguu wawe na subira kuhusiana na lawama wanazopelekewa Waamuzi kutokana na uchezeshaji mbovu unaotokea katika mzunguko mzima wa ligi kuu.
No comments :
Post a Comment