Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, December 10, 2013

WANAHABARI WA ZIARA YA KOMREDI KINANA WAREJEA KWA FURAHA DAR KWA TRENI KUTOKA MAKAMBAKO




 Mmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda akipungia mkono kwa furaha wakati na wanahabari wenzie waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana  katika ziara ya mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe wakiondoka kwa treni la Tazara Makambako kwenda Dar es Salaam jana. Wamwasili leo asubuhi.
 Ni furaha iliyoje kwa wanahabari walipokuwa wakiondoka na msafara wa Komredi Kiwana kwa treni ya Tazara Stesheni ya Makambako, Mkoani Njombe kurejea Dar
 Wanahabari wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakiondoka kwa treni ya Tazara,Makambao kurejea Dar baada ya ziara ndefu ya Kmredi Kinana katika mikowa minne. ambapo wametumia siku 26 na Kinana kuhutubia mikutano zaidi ya 100.
Mmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda (kushoto) akiwa na Afisa wa CCM Makao Makuu, ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya The Nkoromo  wakiwa ndani ya chumba cha Treni ya Tazara wakisafiri kutoka Makambako kwenda Dar.
Wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa Komredi Kinana wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Stesheni ya Tazara, Dar es Salaam

Msondo, Sikinde kupambana Krismasi TCC Club Chang’ombe



Mambo ya Msondo hayoooo...
Na Mwandishi Wetu
Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma “Baba ya Nuziki’ na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  watapambana siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Mpambano huo umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na Konyagi na Nipashe
 Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2013.
 Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itapiga muziki jukwaani kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda.
Wakongwe wa Sikinde, Abdallah Hema (kushoto) na Rehani Bitchuka
“Litakuwa ni pambano la aina yake ukizingatia kila bendi ina vyombo vipya walivyopewa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi). 
Pia tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi majogoo.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja na gazeti la Nipashe, Saluti5 na CXC Africa.

Saturday, December 7, 2013

BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO, KUMSAMBARATISHA DAVID CHALANGA WA KENYA DESEMBA 31



Fransic Miyeyusho
BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake na  David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu mchezo uhu wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakuwa wa raundi nane

Utakuwa chachu kwa mabondia hawo wanaotamba Afrika Mashariki kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki  wa mchezo wa masumbwi kila kona ya tanzania sasa imekuwa gumzo

akizungumzia mpambano huo miyeyusho amesema yeye yupo fiti wakati wowote hule kwani ata sasaivi kama mpinzani wake yuko tayali yeye yupo kwa ajili ya kupigana katika mpambano huo kutakuwa na mapambano ya utangulizi

bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizichapa na Mohamed Kashinde
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

SUPERSHINE MODERN TAARABU YAINGIA KTK 5 BORA ZA MITIKISIKO YA PWANI 2013...!



Kais Mussa Kais (Mzee wa Fitina).
Bendi inayokuja kwa kasi ya ajabu Supershine Modern Taarabu imeweza kuingia katika tamasha la mitikisiko ya pwani 2013 ambalo litafanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala siku ya jumamosi tarehe 14. 

Supershine imeonesha ukomavu mkubwa baada ya kuzipiku bendi zingine kubwa ambazo hazikufanikiwa kuingia katika tamasha hilo.
Bendi ambazo hazikuchagulia ni pamoja na Coast Modern Taarabu, Kings Modern Taarabu, T. Moto na nyinginezo...

Bendi zilizoingia top 5 ni:
Supershine Modern Taarabu, 
Jahazi Modern Taarabu, 
Five Stars, 
East African Melody na Mashauzi Classic

Akizungumza na blog hii ya Taarabu Zetu meneja wa Supershine Kais Mussa Kais ukipenda muite "Mzee wa Fitina" alisema, mwaka huu kulikuwa na ushindani mkubwa sana mchujo ulifanyika zaidi ya mara 2 katika kutafuta ni bendi ipi ya kushiriki tamasha la mwaka huu, lakini kikubwa nawashukuru sana wadau kwa kutuchagua kwa kura zao nasi tunawaahidi burudani nzuri.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA ZANZIBAR






 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua kitambaa kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Bomba kuashiria kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na OMR)

SIASA ZA VURUGU ZINASHUSHA IDADI YA WATALII HIFADHI ZA KASKAZIN





 Watalii  wakipiga  picha katika  wanyama  katika hifadhi ya Taifa ya  Serengeti  mkoani Mara  leo kama  walivyokutwa na  wanahabari  kutoka  mkoa wa Iringa
Mhifadhi  mkuu  wa hifadhi ya  Taifa ya Serengeti  mkoani Mara  Bw  Wiliam Mwakilema  akizungumza na  wanahabari  wa mkoa wa Iringa ambao  wametembelea  hifadhi  hiyo leo

 IMEELEZWA kuwa siasa za vurugu vinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa katika mikoa ya kaskazin zimeendelea kushusha idadi ya watalii katika hifadhi za kaskazin. 

Kauli hiyo imetolewa leo na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti mkoani mara Bw Wiliam Mwakilema wakati akizungumza na timu ya wanahabari 16 kutoka mkoa wa Iringa ambao wametembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kujifunza na kutangaza zaidi vivutio vya utalii 

Mwakilema alisema kuwa moja kati ya mambo yanayokwamisha watalii kufika katika hifadhi ni pamoja na wanasiasa kuendesha siasa za vurugu ambazo zinawatisha watalii hao ambao wengi wanapenda maeneo yasiyo ya vurugu kwa ajili ya kutembelea. 

Bila kuvitaja vyama ama wanasiasa wanaofanya siasa za vurugu Mwakilema aliwataka wanahabari na vyombo vya habari nchini kuendelea kutoa elimu zaidi kwa vyama vya siasa na wanasiasa ili kuepuka kuendesha siasa za vurugu. 

Wakati huo huo Mwakilema alikanusha upotoshwaji unaofanywa na nchi ya Kenya juu ya wanyama aina ya Nyumbu kuwa ni wanyama ambao wanapatikana kenya na kuwa wanyama hao si raia wa Kenya ni wanyama wenye uraia wa Tanzania ambao Kenya wamekuwa wakifika kwa msimu kwa ajili ya malisho na baada ya hapo huzaliana katika hifadhi hiyo ya Serengeti .

MAKAMU WA RAIS DKT. BILALA, MGENI RASMI KWENYE MAGHAFALI YA KWANZA CHUO KIKUU BAGAMOYO






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Petired Bishop Elinasa Sendoro wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Sehemu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Petired Bishop Elinasa Sendoro kulia na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu katikati, wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata keki ya mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013, kulia Mkuu wa Chuo hicho Petired Bishop Elinasa Sendoro, kushoto Makamu Mkuu wa Chuo
Prof. Costa Ricky Mahalu.Picha na OMR

WATANZANIA WAASWA KUHESHIMU HAKI ZA MTOTO






DSC_0960
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Jaji Mstaafu Amir Manento akizungumza na waandishi wa habari wakati mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo hufanyika tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka.
.Jaji Manento asema ni uvunjifu wa sheria kwenda na watoto harusini
Na Damas Makangale, MOblog
WAZAZI na Walezi wameaswa kuacha mara moja tabia ya kwenda na watoto katika sherehe na harusi mbalimbali za kwa sababu ni kosa la Jinai kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto. MOblog inaripoti.
Akizungumza kwenye mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambao huadhimisha kila tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento amesema kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto wazazi au walezi hawaruhusi kwenda na watoto katika sherehe za usiku.
“wazazi na walezi na watu wa kawaida wanamazoea ya kwenda na watoto kwenye sherehe za harusi na majumba ya starehe lakini kwa mujibu wa sheria na haki za mtoto na marekebisho yake ya 2009 ni uvunjifu wa sheria na haki za mtoto,” amesema Jaji Manento.
DSC_0885
Meza Kuu kati kati ni msimamizi (moderator) Dkt Khoti Kamanga toka UDSM, kushoto kwake ni Bw, Godfrey Mulisa toka UN, kushoto mwisho ni Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw, Harold Sungusia na kulia kwa msimamizi ni Francis Nzuki kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala Bora na mwisho kulia ni Bi, Felistas Mushi toka Wizara ya Sheria na Katiba.
Amesema kuwa Tanzania iliridhia tamko rasmi la Haki za Binadamu ili pamoja na mambo mengine kulinda Uhuru na Haki za Binadamu pamoja na haki ya kuishi.
“Tarehe 10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Kuainishwa siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kunakumbusha juhudi kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu Haki za Binadamu kote duniani,” alisisitiza.
Jaji Manento amesema suala la kuheshimiwa haki za binadamu lilipewa kipaumbele cha kwanza wakati wawakilishi wa nchi mbalimbali walipokuwa wakibuni Hati ya Umoja wa Mataifa.
Aliongeza kuwa Januari mwaka 1947 iliundwa kamati ya haki za binadamu na hati ya kamisheni hiyo ilipasishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba 1948.
Jaji manento amesema kuwa kwa msingi huo siku hiyo ya tarehe 10 Disemba ilitambuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu duniani kote.
DSC_0930
Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Harold Sungusia akiwasilisha mada yake kuhusu historia na chimbuko la Haki za Binadamu katika bara la Afrika tangu enzi za miaka 1200 kwenye nchi ya Mali (Mali Empire).
Amesema kuwa imepita zaidi ya miongo sita sasa tangu kutolewa Azimio la Haki za Binadamu ambalo linakusanya thamani za pamoja kwa ajili ya kuondoa ubaguzi, kueneza uhuru na kupambana na dhuluma dhidi ya binadamu duniani.
Alilisitiza kwamba hapana shaka kuwa kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kutimiza lengo hilo ni kazi yenye thamani kubwa. Hata hivyo aliongeza kadhia hiyo inayumbishwa na nchi za Magharibi ambazo zinatumia haki za binadamu na ripoti zinazotolewa na taasisi za haki za binadamu kama nyenzo na fimbo ya kisiasa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea.
Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ni “mafanikio na changamoto katika kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania” .
DSC_1003
Juu na chini ni Baadhi ya vijana wa shule za sekondari mbalimbali na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
DSC_0972
Mjumbe kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora Bw, Francis Nzuki (wa pili kulia) akizungumzia uzoefu wake katika kuhamasisha Haki za binadamu katika Magereza nchini Tanzania hasa kwa Wafungwa.
DSC_0989
Mwakilishi kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bi.Felistas Mushi akiwasilisha mada kuhusu kwanini kuna mpango mkakati wa serikali katika kutekeleza Haki za Binadamu nchini Tanzania.
DSC_1052
Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP akiwahamasisha vijana waliohudhuria mdahalo huo kuwa mstari wa mbele katika kusimamia Haki za Binadamu na kuwaelimisha jamii inayowazunguka kuzitambua Haki zao za msingi.
DSC_1061
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za sheria wa Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora, Bw. Nabor Assey ( wa pili lulia), Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP na Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumziwa kwenye mdahalo huo.
DSC_1025
Pichani Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitoa maoni na kuchangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mdahalo huo.

Friday, December 6, 2013

SEND OFF YA ZENA SELEMANI YAFANA USIKU WA JANA





Zena Selemani kushoto akiwa na mpambe wake wakati wa send off yake
Zena Selemani kulia akiwa na mume wake mtarajiwa anaetarajia kufunga nae ndoa siku ya jumapili ya Desemba 7
Zainabu Mhamila 'Baby Ikota ' katikati katikati akiwa na Zena Selemani pamoja na mpambe wake


Zainabu Mhamila 'Ikota' akiwa na baba yake mzazi Rajabu Mhamila 'Super D
Zainabu Mhamila 'Ikota' akiwa na mama yake mzazi Asha Kamnyanga ' Mama Ikota'

Wazazi wakishudia send off ya mtoto wao kushoto ni Selemani Mrisho na Sikitiko Mohamed
Baadhi ya wakeni waalikwa wakiwa katisha shughuli hiyo

Mwenyekiti wa Kamati ya maandarizi ya Send off hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiselebuka


SUPER D KULIA AKIWA NA IKOTA KATIKATI NA BAADHI YA WANAKAMATI
WAGENI WAALIKWA WAKI PIGA PICHA YA PAMOJA NA MTARAJIWA

MWENYEKITI WA KAMATI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKITAMBULISHA KAMATI YAKE

MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA SEND OFF HIYO RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKITOA NENO LA SHUKRAN
KEKI IKINGIA UKUMBINI KUSHOTO NI ZUHURA,SADA NA ASHA KAMNYANGA 'MAMA IKOTA'

BALOZI SEIF ALI IDDI ATEMBELEA HOTELI YENYE CHUMBA NDANI YA BAHARI "MANTA RESORT " PEMBA ZANZIBAR



Balozi Seif akiwa pembezoni mwa dirisha ndani ya  chumba cha chini ya Bahari akiangalia  samaki na mazingira yake mara baada ya kuuzindua mradi huo hapo Manta Resort Hoteli Makangale.
Balozi Seif akiangalia ngazi ya kutokea juu ya chumba cha chini ya Bahari katika Hoteli ya Manta Resort Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye sherehe za uzinduzi wa chumba hicho ikiwa ni 
muendelezo wa sherehe za kutimia miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Meneja  
Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus  kwa kukamilisha 
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari kwenye hoteli yake iliyopo 
Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba huku Waziri wa Habari Mh. 
Marouk akifurahia kitendo hicho.
Kitanda na mandhari halisi na nzuri iliyomo ndani ya chumba cha chini ya Bahari katika hoteli ya 
Manta Resort Makangale Kaskazini Pemba mradi uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa 
Zanzibar balozi Seif.
Sehemu ya choo katika chumba cha chini ya Bahari kilichopo kwenye Hoteli ya Manta Resort huko Makangale Pemba.
Meneja  Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus Maarufu 
“ Babu kwa Nini  “akitoa maelezo ya hatua zilizochukuliwa kukamilisha 
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari  katika Hoteli ya Manta Resort 
iliyoko Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.Kushoto ya Balozi
 Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Habari, Utamaduni, 
Utalii na Michezo  Mh. Said Ali Mbarouk na Naibu wake Mh. Bihindi Hamad.
Meneja  Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus akionyesha 
eneo la juu la chumba cha chini ya bahari ambapo mgeni atapata fursa ya kupunga upepo pamoja na kuota jua.
Mandhari nzuri ya Hoteli ya Manta Resort ya Makangale Mkoa wa 
Kaskazini Pemba eneo ambalo  kipo chumba cha chini ya Bahari.
Na Othman Khamis Ame  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 

Mradi mpya wa ujenzi wa Chumba cha chini ya Bahari uliofanywa na Hoteli ya Manta Resort iliyopo   katika Kijiji cha Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba umeiweka Zanzibar katika ramani mpya ya Dunia katika harakati za kuimarisha sekta ya Utalii unaobeba nafasi kubwa ya Uchumi katika 
Mataifa mengi Ulimwenguni.